[ad_1]
Vitabu vinavyotolewa na wanasiasa si vya CBC, wizara yaonya
Na ALEX KALAMA
Idara ya Elimu Kaunti ya Kilifi imewaonya walimu wakuu Kaloleni kuhusiana na kudanganywa na wanasiasa wanaogawa vitabu vya masomo ambavyo haviendani na mfumo wa CBC.
Akizungumza kwenye kikao kimoja, kiongozi wa ofisi hiyo Bi Josphine Lomata alisema baadhi ya wanasiasa wanasambaza vitabu ambavyo havijapitishwa na chuo cha maendeleo ya mtaala nchini KICD.
“Kuna vitabu vinapeanwa humu humu na kitabu chochote ni lazima kipitie kwa ofisi ya idara ya elimu tuone kama ni kitabu ambacho kimeidhinishwa. Kwa hivyo wewe huko nje ukipewa vitabu textbooks ambazo havijaidhinishwa unajua saa hii tunafanya CBC na wewe uletewe kitabu cha 8-4-4 ambacho kimepitwa na wakati.
“Tafadhali hii ninasema kila mtu asikie tusikubali kuchukua vitabu ambavyo havijahalalishwa na KICD kupitia kwa wizara ya elimu kwa hivyo tuangalie hayo,” alisema Bi Lomata.
Kulingana na afisa huyo wa elimu amewataka wenyeji wa eneo hilo la Kaloleni na kaunti ya Kilifi kwa jumla kuwapeleka shule watoto wao ili wanufaike na elimu na kuweza kujisaidia katika maisha ya baadaye.
“Ningependa kuwaomba wazazi na kusisitiza ya kwamba elimu ndio mambo yote,tupeleke watoto shule ningependa kusisitiza hilo. Kwa hivyo wazazi nina wasisitizia tupeleke watoto hakuna kufukuza watoto nimetangulia kusema elimu ni ya bure serikali imetoa elimu ya bure.
“Kwa hivyo mambo ya kila wakati watoto wanaonekana mitaani wanarandaranda ovyo ovyo hatutaki kuanzia leo na kuendelea mbele watoto wakae shule wasome,” alisema Bi Lomata.
Hata hivyo afisa huyo wa elimu alidokeza kuwa baadhi ya shule zilizoko katika eneo bunge hilo bado zinakumbwa na tatizo la uhaba wa walimu hususani shule za upili.
Aidha pia alidokeza kuwa kuna haja ya serikali ya kitaifa kuweka mikakati itakayosaidia kuinua viwango elimu eneo hilo.
Next article
Pwani yawapa Raila na Ruto masharti makali
[ad_2]
Source link