Connect with us

General News

Waasi kuhama Ford-K ni dafrau kwa Wetangula – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waasi kuhama Ford-K ni dafrau kwa Wetangula – Taifa Leo

JAMVI: Waasi kuhama Ford-K ni dafrau kwa Wetangula

MZOZO ndani ya chama cha Ford Kenya utafikia kilele Jumanne pale mrengo unaoongozwa na mbunge wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi utakapokigura rasmi na kujiunga na chama kingine cha kisiasa.

Wadadisi wanasema hatua hiyo ni pigo kwa chama hicho ambacho ni chama kongwe zaidi cha upinzani nchini. Kiliasisiwa na aliyekuwa shujaa wa ukombozi wa pili nchini marehemu Jaramogi Oginga Odinga. Hii ni kwa sababu waasi hao wanatarajiwa kuondoka pamoja na wanachama waaminifu kwaoWiki jana, Bw Wamunyinyi na mwenzake wa Tongaren Eseli Simiyu walitangaza kuwa watahama chama hicho cha Simba na kujiunga na chama ambacho watakitumia kushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Juhudi za wawili hao kutwaa udhibiti wa chama hicho ziliambulia patupu mwezi jana baada ya Afisi ya Msajili Mkuu wa Vyama vya Kisiasa Anne Nderitu kumtambua Seneta wa Bungoma Moses Wetang’ula kama kiongozi rasmi wa Ford Kenya.

Mnamo Novemba mwaka jana bw Wamunyinyi na Dkt Simiyu walijaribu kumng’oa mamlakani Bw Wetang’ula lakini juhudi hizo zikaaambulia patupu mahakama kuharamisha mapinduzi hayo.Japo wamedinda kutaja jina la chama hicho, duru zimeeleza meza ya ‘Jamvi la Siasa’, kwamba wanasiasa hao wanapania kujiunga na chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP) kinachohusishwa na Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa.

Inasemekana kuwa chama kitashirikiana na vuguvugu la Azimio la Umoja linaloongozwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga.“Tutazindua chama kipya ambacho kitaendeleza maslahi ya watu wetu katika kaunti za Bungoma na Trans Nzoia na sehemu zingine nchini,” Bw Wamunyinyi akasema.

Kwa upande wake Dkt Simiyu akasema: “Mwenda wazimu akichukua nguo zake unapooga mtoni, haumfuati ukiwa uchi. Unajifunika kwa matawi ya miti kisha unatafuta nguo mpya. Kwa hivyo tumepata nguo mpya.”Kwenye mahojiano na safu hii, wabunge hao walifichua kuwa viongozi wa matawi 32 ya Ford Kenya kote nchini wataungana watakapojiounga na chama kipya.

“Ningependa kuwahakikishia Wetang’ula na wenzake kwamba Ford Kenya itasalia mahame. Chama hicho kinaelekea kuzikwa katika kaburi la sahau kutokana na uongozi mbaya wa Wetang’ula na washirika wake,” akasema Bw Wamunyinyi huku akitoa wito kwa wafuasi wa chama hicho kuungana nao katika chama kipya.

Naye Bw Eseli ambaye hadi mwezi jana alishikilia wadhifa wa Katibu Mkuu katika Ford Kenya, alisema waliamua kuhama chama hicho baada ya Bw Wetang’ula kugeuka kuwa kibaraka wa Naibu Rais William Ruto.

“Hatukutaka kuwa sehemu ya mrengo ambao unapania kurejesha taifa hili nyuma kimaendeleo na kiuongozi kwa kujiunga na kambi ya Ruto,” akaelezaMchanganuzi wa masuala ya kisiasa Martin Andati anasema hatua ya wabunge hao kuhamia chama kingine cha kisiasa ni pigo kwa mrengo wa Bw Wetang’ula.

“Hii ni kwa sababu wanasiasa hawa pia wana wafuasi wao, ilivyoshuhudiwa Novemba mwaka jana walipojaribu kumng’oa mamlakani Bw Wetang’ula,” anaeleza.Lakini katibu mratibu wa Ford Kenya Chris Mandu amepuuzilia mbali hatua ya Bw Wamunyinyi na Dkt Eseli kugura Ford Kenya akisema hatua hiyo haitadhoofisha chama hicho.

“Uamuzi wao kuondoka hauna athari zozote kwetu. Tayari walikuwa wamefurushwa kutokana na jaribio lao la kutekeleza mapinduzi ya uongozi chamani mwaka jana. Tunawakia kila la kheri wanakokwenda,” akasema, akiongeza kuwa Bw Wetang’ula angali na ushawishi mkubwa eneo la magharibi na taifa kwa ujumla.

Bw Mandu adai kuwa jaribio la mapinduzi lililotekelezwa na wawili hao lilichochewa na kufadhiliwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga.“Hawa watu wanaelekea kwa Raila ambaye amekuwa akiwatumia kuhujumu uongozi wa chetu kwa manufaa yake kibinafsi.

Kesho (Ijumaa) utawaona kule Kasarani katika mkutano wa Azimio la Umoja, ambao sisi hatutadhuria,” akaeleza afisa huyo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending