Connect with us

General News

Wabunge kujadidli kero la watu kuuawa na miili yao kutupwa Mto Yala – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wabunge kujadidli kero la watu kuuawa na miili yao kutupwa Mto Yala – Taifa Leo

Wabunge kujadidli kero la watu kuuawa na miili yao kutupwa Mto Yala

Na CHARLES WASONGA

WABUNGE watapata nafasi wiki ijayo ya kujadili kero la miili ya watu waliouawa kwingine na kutupwa kando ya Mto Yala, eneobunge la Gem, Kaunti ya Siaya.

Akiongea na wanahabari Ijumaa katika majengo ya bunge, Mbunge wa Gem Elisha Odhiambo alisema atawawasilisha ombi bungeni kwa niaba ya wakazi wa Yala kuitaka Wizara ya Usalama itanzue kitendawili hicho.

“Mnamo Alhamis wiki ijayo, nitawasilisha ombi bungeni nikitaka uchunguzi wa kina ufanywe kwa lengo la kubaini kiini cha kutupwa kwa miili ya katika Mto Yala. Kupitia Kamati ya Bunge kuhusu Usalama, nitataka maelezo kutoka kwa Afisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi na Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kuhusu uovu huo,” Bw Odhiambo akasema.

Kulingana na kanuni za bunge, wabunge hupewa muda wa dakika 30 kuzunguzia taarifa za maombi zinazowasilishwa na wenzao katika kikao cha bunge lote.

Baada ya masuala yaliyoangaziwa na wabunge kujadiliwa kwa kifupi, huwasilishwa kwa kamati husika ambayo hualika waziri husika kuelekeza hatua ambayo wizara yake inachukua kuyashughulikia.

Bunge linarejelea vikao vyake rasmi Jumanne, Januari 25, 2022 baada ya likizo ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Mapema wiki hii kamanda wa polisi katika Kaunti Ndogo ya Gem Charles Chacha alisema kuwa maafisa wake pia wameshangazwa na ongezeko la maiti zinazopatikana zimetupwa kando ya Mto Yala.

Bw Chacha alisema kuwa kuanzia Januari 2021 hadi wakati huu, polisi wameopoa miili 11, mingi ikiwa imetupwa karibu na Ndanu Falls.

“Nyingi za maiti hizo huwa zinapatikana zimekwama karibu na Ndanu Falls,” akasema kamanda huyo.

Bw Chacha alisema baadhi ya miili hiyo imehifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Yala Level 5, mjini humo.

Alisema polisi wameanzisha uchunguzi uhalifu huo huku akitoa wito kwa wakazi ambao jamaa zao wametoweka kufika katika kituo cha polisi cha Yala kupata usaidizi.

“Miili ambayo imeoza zaidi kiasi cha kutotambulika itafanyiwa uchunguzi wa DNA kwa ajili ya kuitambua,” Bw Chacha akasema.

Afisa huyo alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu ambao miili yao hutupa kando ya mtu huo huwa wameaua kwingineko wala sio maeneo ya karibu.

Hata hivyo, mkurugenzi wa shirika la kutetea haki, Haki Africa Hussein Khalid aliyezuru aneo hilo alisema zaidi ya miili 20 imeopolewa kutoka mto huo tangu Agosti mwaka jana.

Bw Khalid ambaye alizuru eneo la tukio mapema wiki hii aliitaka serikali kutanzua kitendawili kuhusu uhalifu huo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending