Connect with us

General News

Wabunge walionyesha mfano mbovu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wabunge walionyesha mfano mbovu – Taifa Leo

TAHARIRI: Wabunge walionyesha mfano mbovu

NA MHARIRI

JUMA lililopita wabunge walionyesha mwenendo mbovu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Kenya walipoangusha hoja muhimu inayohusu maslahi ya taifa zima kwa ubinafsi wao.

Wabunge wanaoegemea mrengo wa Tangatanga waliangusha hoja ya kuidhinisha kamati iliyoteuliwa kuendesha shughuli za Bunge ambayo pia hushughulikia maandalizi ya bajeti.

Ilibidi Kiongozi wa Wengi, Bw Amos Kimunya awasilishe ombi la kubatilisha uamuzi huo kisha Spika Justin Muturi akaitisha kikao kingine jana ambacho hatimaye kiliidhinisha kamati hiyo muhimu.

Iwapo uamuzi wa wabunge hao wanaoegemea mrengo wa Tangatanga ungeachwa kudumu, ina maana kuwa mwaka huu taifa hili halingekuwa na bajeti, hali ambayo ingeathiri taifa hili zima wakiwemo wao waliohusika katika kuiangusha hoja hiyo.

Mtu mwenye fikra za wastani tu anapotazama uamuzi wa aina hiyo hasiti kujiuliza iwapo watu wa aina hiyo walikuwa wanatumia akili au ‘tope’ katika bongo zao.

Je, ilikuwa vigumu kuona matokeo ya uamuzi wao huo?

Kwa upande wetu raia tunaowakilishwa nao, tunaweza kujiuliza, je hawa ndio watu wanaolipwa mshahara kutokana na ushuru wetu tunaotozwa ilhali wanakataa kupitisha harakati muhimu na ya kimsingi kama hii?

Ukweli ni kwamba wabunge hao walikuwa wanaongozwa na siasa za ubabe na jazba za ushindani badala ya kutumia busara waliyopewa na Maulana.

Viongozi wa sampuli hii kwa hakika hawafai kurejeshwa bungeni katika uchaguzi mkuu ujao maadamu hawana wanalotufaa.

Wazo hili halijachochewa na mrengo wowote wa kisiasa bali ukweli kwamba viongozi wetu wa siasa wanaweza kuruhusu mihemko ya kisiasa iliyopo kuwaongoza kutuelekeza katika hali mbovu inayoweza kutudhuru.

Kutopitishwa kwa bajeti ni sawa na kukwamisha maisha ya raia wote wa Kenya ikiwemo ulipaji madeni; hali inayoweza kuchangia kunadiwa kwa taifa hili.

Hali kama hii ndiyo iliyomuongoza Seneta wa Meru Mithika Linturi aliyetamka maneno ya uchochezi aliyokuja ‘kujutia’ baadaye.

Wanasiasa katika hali kama hii huongozwa na jazba badala ya kuongozwa na urazini bila kujali matokeo yake ambayo wakati mwingine huwa hatari zaidi.

Kwa mantiki hiyo itakuwa bora wanasiasa wanapozama katika kampeni kipindi hiki kilichosalia kabla ya uchaguzi wa Agosti 9, wamakinike zaidi wasije wakaongozwa na hisia badala ya bongo zao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending