Wachezaji wa EPL na WSL watamalaki orodha ya wawaniaji wa tuzo za FIFA 2020-21
Na MASHIRIKA
CRISTIANO Ronaldo wa Manchester United, Mohamed Salah wa Liverpool pamoja na wanasoka wawili wa kike wa Manchester City – Ellen White na Lucy Bronze ni miongoni mwa masogora ambao wameteuliwa kuwania tuzo za Wanasoka Bora wa FIFA 2021.
N’Golo Kante na Jorginho wa Cheslea pia wanaunga orodha ya wanasoka wa kiume ambayo inamjumuisha vilevile nyota wa Man-City, Kevin de Bruyne. Vipusa wa Chelsea – Magdalena Eriksson, Pernille Harder, Ji So-yun na Sam Kerr pia wanaunga orodha ya kina dada kwa pamoja na Vivianne Miedema wa Arsenal.
Emma Hayes wa Cheslea atawania tuzo ya Kocha Bora baada ya kuongoza waajiri wake kutinga fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Atamenyana na Sarina Wiegman wa timu ya taifa ya Uingereza na kocha mzawa wa Uingereza na raia wa Canada, Beverly Priestman.
Mkufunzi Pep Guardiola wa Man-City, Thomas Tuchel wa Chelsea na Antonio Conte wa Tottenham Hotspur watawania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka. Orodha ya wawaniaji wa tuzo ya Mwanasoka Bora inatamalakiwa na wachezaji wa Ligi Kuu ya Uingerez kwa upande wa wanaume (EPL) na upande wa wanawake (WSL).
Wawaniaji saba kati ya 13 wa kike pamoja na watano kati ya 11 wa kiume wanasakata soka nchini Uingereza. Alisson Becker wa Liverpool, Edouard Mendy wa Chelsea na Kasper Schmeichel wa Leicester City watapambania taji la Kipa Bora.
Ann-Katrin Berger wa Chelsea anaunga orodha ya wawaniaji wa taji la Kipa Bora kwa upande wa wanawake. Tuzo hiyo itatolewa kwa matokeo bora ya wachezaji katika ngazi ya klabu ba timu za taifa kati ya Oktoba 8, 2020 na Agosti 6, 2021.
Washindi watakaotangaza Januari 17, 2022, watapigiwa kura na manahodha, makocha, wanahabari na umma.
Mchezaji Bora wa Kike:
§ Stina Blackstenius (Uswidi/BK Hacken)
§ Aitana Bonmati (Uhsipania/Barcelona)
§ Lucy Bronze (Uingereza/Manchester City)
§ Magdalena Eriksson (Uswidi/Chelsea)
§ Caroline Graham Hansen (Norway/Barcelona)
§ Pernille Harder (Denmark/Chelsea)
§ Jennifer Hermoso (Uhispania/Barcelona)
§ Ji So-yun (Korea Kusini/Chelsea)
§ Sam Kerr (Australia/Chelsea)
§ Vivianne Miedema (Uholanzi/Arsenal)
§ Ellen White (Uingereza/Manchester City)
§ Alexia Putellas (Uhispania/Barcelona)
§ Christine Sinclair (Canada/Portland Thorns)
Mchezaji Bora wa Kiume:
§ Karim Benzema (Ufaransa/Real Madrid)
§ Kevin de Bruyne (Ubelgiji/Manchester City)
§ Cristiano Ronaldo (Ureno/Juventus/Manchester United)
§ Robert Lewandowski (Poland/Bayern Munich)
§ Lionel Messi (Argentina/Barcelona/Paris Saint-Germain)
§ Neymar (Brazil/Paris Saint-Germain)
§ Erling Braut Haaland (Norway/Borussia Dortmund)
§ Jorginho (Italia/Chelsea)
§ N’Golo Kante (Ufaransa/Chelsea)
§ Kylian Mbappe (Ufaransa/Paris Saint-Germain)
§ Mohamed Salah (Misri/Liverpool)
Kocha Bora wa Kike:
§ Lluis Cortes (Uhispania/Barcelona)
§ Peter Gerhardsson (Uswidi/Swedish national team)
§ Emma Hayes (Uingereza/Chelsea)
§ Beverly Priestman (Uingereza/Canadian national team)
§ Sarina Wiegman (Uholanzi/Timu ya taifa ya Uholanzi/Timu ya taifa ya Uingereza
Kocha Bora wa Kiume:
§ Antonio Conte (Italia/Inter Milan/Tottenham Hotspur)
§ Hansi Flick (Ujerumani/Bayern Munich/Timu ya taifa ya Ujerumani)
§ Pep Guardiola (Uhispania/Manchester City)
§ Roberto Mancini (Italia/Timu ya taifa ya Italia)
§ Lionel Sebastian Scaloni (Argentina/Timu ya taifa ya Argentina)
§ Diego Simeone (Argentina/Atletico Madrid)
§ Thomas Tuchel (Ujerumani/Chelsea)
Kipa Bora wa Kike:
§ Ann-Katrin Berger (Ujerumani/Chelsea)
§ Christiane Endler (Chile/Paris Saint-Germain/Lyon)
§ Stephanie Lynn Marie Labbe (Canada/FC Rosengard/Paris Saint-Germain)
§ Hedvig Lindahl (Uswidi/Atletico Madrid)
§ Alyssa Naeher (Amerika/Chicago Red Stars)
Kipa Bora wa Kiume:
§ Alisson Becker (Brazil/Liverpool)
§ Gianluigi Donnarumma (Italia/AC Milan/Paris Saint-Germain)
§ Edouard Mendy (Senegal/Chelsea)
§ Manuel Neuer (Ujerumani/Bayern Munich)
§ Kasper Schmeichel (Denmark/Leicester City)
Next article
Wakenya wachanjwe, lakini si kwa vitisho – Amnesty…