Connect with us

General News

Wafanyakazi wa Kenya Power motoni kwa wizi wa vifaa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wafanyakazi wa Kenya Power motoni kwa wizi wa vifaa – Taifa Leo

Wafanyakazi wa Kenya Power motoni kwa wizi wa vifaa

Na LAWRENCE ONGARO

WAFANYAKAZI wanne wa kampuni ya umeme ya Kenya Power walifikishwa katika mahakama ya Thika kwa makosa ya kuwa na vifaa vya kampuni hiyo bila idhini.

Bw David Muriithi Githinji, Henry Mbae, Jackson Thuo Macharia, na Jared Juma, walikanusha mashataka matatu walipofikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Thika, Bi Vicky Kachuodho.

Washtakiwa walifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali huku wakiinamisha vichwa vyao chini ili wasitambilike na yeyote.

Shtaka la kwanza ni kwamba kati ya tarehe 26- 27, Januari, 2022, washtakiwa hao pamoja na watu wengine walichomoa transfoma yenye thamani ya Sh 1.2 milioni eneo la chuo cha Kilimambogo Teachers’ Training College katika eneo la Thika Mashariki.

Shtaka la pili ni kwamba kati ya tarehe 21 na 22 mwezi Februari, 2022, eneo la Gatiiguru, Thika Mashariki, waliiba Transfoma ya kampuni ya umeme ya KPLC yenye dhamani ya Sh 700,000.

Shtaka la tatu lilieleza kuwa Kati ya Disemba Mosi, mwaka wa 2021 na Machi 5, 2022, washtakiwa wote wanne walipokea pesa ya dhamani ya Sh 908,610 zilizotumiwa kupitia M- pesa kutoka kwa Patrick Muchemi baada ya kuuziwa vifaa vya kampuni ya KPLC.

Washtakiwa mahakama ilijulishwa walikamatwa mnamo April, 7, 2022 baada ya kupatikana na vifaa hivyo vilivyoibwa katika wakati tofauti.

Washtakiwa waliposomewa mashataka walikanusha, huku wakiwa wameficha nyuso zao zisionekane.

Hakimu Bi Kachuodho aliamuru washtakiwa wazuiliwe kwenye seli kwa muda wa siku 21 huku uchunguzi ukiendelea.

Kesi hiyo imepangwa kutajwa mnamo April 29, 2022.