– Chanzo chetu kilisema idadi ya waliohudhuria shereheilikuwa kubwa ushinda idadi ya watu 15 wanaoruhusiwa na serikali
– Pia sherehe ilifanyika usiku kuchwa katika nyumba ya Stephen Letoo na hvyo walivunja sheria za kafyu
– Mmoja wa waliohudhuria alikuwa na dalili za COVID-19 na baada ya kupimwa alipatikana na virusi vya ugonjwa huo
– Letoo alikuwa mtu wa pili kukutwa na virusi hivyo baada ya vipimo Nairobi Hospital
Imebainika kuwa nyumba ya mwanahabari wa Citizen TV Stephen Letoo ilihudhuriwa na mtu aliyekuwa akiugua COVID-19 wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mwanawe wa kiume na hivyo kusababisha wangeni wengine kuambukizwa ugonjwa huo.
Mtu wa karibu wa familia hiyo amesema marafiki wa Letoo, wakiwamo kutoka Royal Media Services wamekutwa na virusi vya ugonjwa huo huku wengine wakisubiri matokeo ya vipimo.
Matokeo hayo yalimfanya mwanahabari huyo kuenda Nairobi Hospital mnamo Jumatano, Julai 15, na matokeo yalionyesha alikuwa ameambukizwa virusi hivyo. Mwingine aliyeambukizwa ni rafiki wa kiume wa Letoo, aliyepimwa katika Hospitali ya Mbagathi, chanzo kilisema.
Vile vile, imebainika kuwa, baadhi ya waliokuwa kwenye sherehe tayari walisafiri na kurejea mikoani.
“Kuna walioondoka Nairobi, mmoja kutoka Kilgoris na mwingine Narok. Inasikitisha kwa kuwa wanatangamana na watu ingawa waetakiwa kijitenga,” chanzo chetu kilisema.
Kulingana na chanzo hicho, waliohudhuria walivunja kanuni kadha za Wizara ya Afya kuhusu kujikinga dhidi ya maradhi ya COVID-19.