Connect with us

General News

Wakazi wa mitaa sita ya Mukuru wahangaika kupata maji kwa zaidi ya wiki moja – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakazi wa mitaa sita ya Mukuru wahangaika kupata maji kwa zaidi ya wiki moja – Taifa Leo

Wakazi wa mitaa sita ya Mukuru wahangaika kupata maji kwa zaidi ya wiki moja

Na SAMMY KIMATU

WAKAZI katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kwa Reuben ulioko katika kaunti ndogo ya Embakasi Kusini wanahangaika kwa kukosa maji kwa siku ya nane mfululizo.

Tangu wiki jana, mifereji imekauka mtaani na kukosesha wenyeji usingizi wakisaka maji.

Isitoshe, maji wanayotegemea kutoka kwa visima vilivyochimbwa na Shirika la Huduma Jijini Nairobi (NMS) hayakuwepo kutokana na kuharibika kwa pampu.

Kando na hayo, mitaa jirani ya Mukuru- Tetra Pak na Mukuru-Kingstone kwenye kaunti ndogo ya Makadara ilikumbwa na uhaba wa maji pia.

Uhaba huu pia umeikumba mitaa ya mabanda wa Mukuru-Kayaba, Mukuru-Hazina na Mukuru-Maasai.

Hata hivyo, wenyeji walipata afueni kwa kupata huduma ya maji katika kisima cha NMS katika kambi ya chifu iliyoko katika mtaa wa Hazina.

“Tunahangaika kwa kukosa maji ya kunywa na ya matumizi mengine nyumbani, saluni, vibanda vya vyakula, bucha na maeneo mengine,” Bi Mary Mutuku akanena.

Mhandisi kutoka kampuni ya kusambaza maji kaunti ya Nairobi ambaye haruhusiwi kuongea na wanahabari alidokeza kwamba tatizo hilo lilichangiwa na ubadilishaji wa paipu mkabala wa barabara ya Mombasa.

“Ujenzi wa barabara mpya ya kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kuelekea Westlands uliathiri usambazaji wa maji kwa muda wote huo. Huduma za kawaida zitarejea kuanzia leo (Jumatatu),” mhandisi akaambia Taifa Leo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending