Connect with us

General News

Wakazi wasema ni unafiki kwa wanasiasa kuzungumzia Bandari

Published

on

Wakazi wasema ni unafiki kwa wanasiasa kuzungumzia Bandari

WAKAZI wa Mombasa wakiongozwa na mashirika ya kijamii wamewakashifu wanasiasa kwa kujifanya kujali maslahi yao wakati wa kampeni za uchaguzi wa Agosti.

Wametaka viongozi wa kisiasa kukoma kujadili suala la mfumo wa kusimamia shughuli za bandari na huduma za reli ya SGR, wakisema wengi wao si waaminifu.

“Walikuwa wapi wakati suala zima lilikuwa likijadiliwa? Nakumbuka tulifanya maandamano kila Jumatatu tukirai serikali kuregesha huduma hizo, ila wanasiasa walitupuuza. Ni sasa ambapo wanatafuta kura zetu ndio wanatuahidi watarejesha. Hatuna imani kama jamii kwamba watarejesha shughuli za bandari yetu jinsi iliyvokuwa awali,” alisema Bi Naila Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Sisters for Justice.

Aliungwa mkono na Afisa wa Masuala ya Dharura wa shirika la Muslims for Human Rights (Muhuri), Bw Francis Auma.

Bw Auma alisema kunahitajika kuwepo mpangilio mbadala utakaohakikisha Kaunti ya Mombasa inanufaika kwa mapato ya bandari, na pia mipango ya kuongeza ajira kwa vijana.

Comments

comments

Trending