Connect with us

General News

Wakenya sasa warejea kazini kupambana na changamoto za 2022 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakenya sasa warejea kazini kupambana na changamoto za 2022 – Taifa Leo

Wakenya sasa warejea kazini kupambana na changamoto za 2022

BENSON MATHEKA NA PHILIP MUYANGA

BAADA ya msimu wa sherehe za mwisho na mwanzo wa mwaka, Wakenya wameanza kurudia shughuli zao za kawaida.

Jana, walikusanyika katika maeneo ya kuabudu kushukuru na kuomba Mungu huku waliokuwa wamesafiri kuungana na jamaa zao wakisafiri kurudi mijini.

Viongozi wa kidini walihimiza Wakenya kudumisha amani na kumtumainia Mungu katika shughuli zao za maisha mwaka huu.

Katika eneo la Pwani, wakazi walimiminika katika fuo kukamilisha sherehe za mwaka mpya kabla ya kuanza shughuli za kawaida za uchumi leo.

Vituo vya magari ya uchukuzi wa umma kote nchini vilikuwa na shughuli nyingi watu wakiwa katika pilkapilka za kusafiri na wahudumu wa matatu wakipandisha nauli.

“Ninasafiri hadi Mombasa ili kuandaa watoto wangu wanaofungua shule kesho kabla ya kurejea kazini baadaye Jumatano,”alisema Jane Muoki, mjini Machakos aliyeandamana na watoto wake wawili.

Alisema alikuwa amejiandaa kwa lolote kwani alitarajia nauli kupanda.Baadhi ya wakazi walisema japo hali ya maisha ni ngumu, wanachoomba ni uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kukosa ghasia.

“Nina matumaini ya kuwa mwaka wa 2022 utakuwa bora,ninaomba uchaguzi uwe bila vurugu yeyote na wakenya wote tuweze kuishi kwa amani,”alisema mwanamke aliyejitambulisha kama Grace mjini Mombasa.

Mzee Abdulrahman Abdallah mkaazi wa majengo alilamikia kupandishwa kwa bei ya bidhaa kama vile unga na mkate.

“Mwaka wa 2022 tunaomba serikali iweze kupunguza bei ya bidhaa za matumizi ya kila siku nyumbani,” alisema Mzee Abdallah.

“Mwaka wa 2022 tunaomba serikali iweze kupunguza bei ya bidhaa za matumizi ya kila siku nyumbani,” alisema Mzee Abdallah.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending