Connect with us

General News

Wakenya wachanjwe, lakini si kwa vitisho – Amnesty International – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakenya wachanjwe, lakini si kwa vitisho – Amnesty International – Taifa Leo

Wakenya wachanjwe, lakini si kwa vitisho – Amnesty International

Na WANGU KANURI

SHIRIKA la kimataifa linalotetea haki za kibinadamu, Amensty International, limeirai serikali ya Kenya dhidi ya kuwatishia wananchi ambao hawajapata chanjo za Covid-19.

Katika ujumbe kwa wanahabari, Mkurugenzi Mtendaji wa Amensty, Irungu Houghton, aliishawishi serikali ya Kenya kuwaelimisha Wakenya badala ya kutumia vitisho.

“Hata ingawa kuna sababu halali za afya ya umma, sababu hizo hazipaswi kumnyima mtu haki ya kufanya kazi, kupata huduma muhimu kama elimu, afya na ulinzi au pia kuwakataza watu kusafiri,” akaeleza.

Vile vile, Bw Houghton alieleza kuwa nchi nyingi zilizoweka masharti katika maeneo ya umma na ya kibinafsi zimewachanja watu asilimia 60-70. Asilimia hiyo itakuwa ngumu kwa Kenya kufikia kwa mwezi mmoja kwani kwa sasa Kenya imewachanja watu asilimia 8.8.

Mwito kutoka Amensty unajiri siku chache baada ya Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kutangaza kuwa Wakenya hawatapokea huduma za kiserikali iwapo hawatakuwa wamepokea chanjo kamili ifikiapo Desemba 21, 2021.

Tisho zake Waziri Kagwe ziliibua gumzo mitandaoni huku Wakenya wakishikilia kuwa iwapo watanyimwa huduma za kiserikali, basi wasiombwe kura. Wizara ya Afya inanuia kuwachanja watu nusura milioni 10 ifikiapo mwisho wa Desemba.

Hata hivyo, ni watu milioni 6.4 ndio wamechanjwa nchini ilhali watu milioni 2.4 wakiwa wamepata chanjo kamili.

Waziri Kagwe alitangaza kuwa kampeni ya kuwachanja watu itaanzia Novemba 26, 2021 na itakuwepo kwa siku kumi. Kampeni hiyo inanuia kuongezea idadi ya watu waliochanjwa nchini.