[ad_1]
Wakenya waenda Tanzania kusaka mafuta
Na SIAGO CECE
UHABA wa mafuta katika Kaunti ya Kwale umewalazimu madereva kusafiri hadi Tanzania kupitia mpaka wa Lungalunga ili kutafuta bidhaa hiyo muhimu, huku wafanyabiashara wakipandisha bei kutokana na uhaba mkubwa nchini.
Uchunguzi wa Taifa Leo uligundua vituo vingi vya mafuta katika miji ya Kwale na Ukunda havikuwa na dizeli na petroli.
Rasilimali hiyo ilipatikana tu katika vituo vikubwa vya mafuta katika kaunti za mpakani. Foleni ndefu pia zilikuwa zimepangwa hasa nyakati za asubuhi na jioni wakati madereva wa magari walikimbilia kujaza mafuta kwenye gari.
‘Tumeambiwa kuwa kuanzia kesho, kunaweza kusiwe na mafuta ndiyo maana nataka kuhakikisha najaza tanki langu ili niendelee kufanya biashara,’ alisema Abdalla Kalama, dereva wa Tuktuk huko Ukunda.
Hali hiyo pia imezua tatizo la usafiri katika maeneo ya mijini kama vile Ukunda ambapo nauli zimepanda kwa Sh10 na Sh20. Madereva wa magari sasa wanatutumia mpaka wa Lungalunga kupata mafuta kwa bei nafuu nchini Tanzania.
Next article
Polisi wamechoka na siasa za mapema, Matiang’i alalamika
[ad_2]
Source link