Connect with us

General News

Wakenya wangali wamegawanyika licha ya ahadi ya handisheki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakenya wangali wamegawanyika licha ya ahadi ya handisheki – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Wakenya wangali wamegawanyika licha ya ahadi ya handisheki

SIKU kama ya leo mnamo Machi 9, 2018 Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga walizika tofauti zao za kisiasa kwa kusalimiana nje ya Afisi ya Rais iliyoko jumba la Harambee, Nairobi.

Wawili hao aliwaambia Wakenya kwamba waliweka tofauti zao zilizotokana na uchaguzi wa urais wa Agosti 8, 2017 ambao matokeo yake yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu iliyoamuru shughuli hiyo irudiwe.

Rais Kenyatta na Bw Odinga waliwaambia Wakenya kwamba maridhiano yao, maarufu kama handisheki, hayakuwa kwa ajili ya siasa za urithi wa urais 2022, bali kuunganisha Wakenya waliokuwa wamegawanyika kwa misingi ya kisiasa.

Lakini sasa, miaka minne baadaye, tusisahau kuwa taifa lingali limegawanyika kwa misingi mingi ya kisiasa na kikabila na Rais Kenyatta amemwidhinisha Bw Odinga kama chaguo lake katika kinyang’anyiro cha urais Agosti 9, 2022.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending