Connect with us

General News

Wakenya wapewa muda zaidi kujiandikisha katika ofisi za IEBC – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakenya wapewa muda zaidi kujiandikisha katika ofisi za IEBC – Taifa Leo

Wakenya wapewa muda zaidi kujiandikisha katika ofisi za IEBC

NA CHARLES WASONGA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetoa nafasi nyingine kwa Wakenya kujiandikisha kuwa wapiga kura kupitia afisi zake zilizoko maeneo bunge 290 nchini.

Hii ni baada ya tume hiyo kuandikisha idadi ndogo ya wapiga kura wapya katika awamu ya pili iliyokamilika Jumapili.

Kwenye taarifa kwa vyombo habari, mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema walifanikiwa kusajili wapiga wapya 1,031,645 pekee ilhali walilenga watu 4.5 milioni.

“Hata hivyo, wale ambao hawajajisajili kufikia siku ya mwisho ya awamu Februari 6, 2022 wanashauriwa kufika kati – ka ofisi za IEBC katika maeneo bunge ili wasajiliwe. Hii itakuwa fursa nyingine kwa Wakenya ambao walipata vitambulisho vyao vya kitaifa baada ya shughuli kufungwa,” Bw Chebukati akasema.

Kulingana mwenyekiti huyo, mitambo miwili ya usajili kieletroniki (BVR) itawekwa katika ofisi za IEBC katika kila moja ya maeneo bunge 290 nchini.

“Vifaa hivyo pia vitawekwa katika vituo vya Huduma Centre kote nchini ambako Wakenya wanaweza kuendelea kujiandikish,” akaongeza.