Connect with us

General News

Wakili adai harudishi pesa alizotumiwa na Mungu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Ijumaa iliamuru kesi inayohusu Sh1.5milioni kati ya wakili na mteja wake iamuliwe na mpatanishi ilipoelezwa mwanasheria huyo alipokwamilia pesa za mlalamishi akisema, “ kamwe siwezi rudisha pesa hizo kwa vile nilitumiwa na Mungu kwa akaunti yake ya benki.”

Wakili Alphaxard Osoro Mogikoyo anayeshtakiwa kwa wizi wa Sh1.5milioni zilizotumwa kimakosa kwa akaunti yake  na Christopher Onunga Oanda adaiwa alieleza kamati maalum ya Kanisa la SDA Karengata  hatarudisha pesa hizo kwa vile alitumiwa na Mungu.

Baada ya kusikia wawili hao walikuwa wamewashirikisha Pasta na Wazee wa Kanisa kuwapatanisha, hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi aliamuru idara ya upatanishi ya korti imteue mpatanishi atakayesimamia kamati ya kuwapatanisha Mogikoyo na Oanda.

Kesi hiyo ilizua vioja kadhaa huku Bw Oanda akidai Mogikoyo sio wakili hatekelezi majukumu yake barabara inavyompasa mwanasheria.“Mheshimiwa tuko mbele ya hii mahakama kwa sababu ya wakili kutotekeleza majukumu yake ipasavyo,”alisema Oanda.

Aliendelea kumweleza Bw Andayi kama Bw Mogikoyo angelimrudishia pesa zake hangelimshtaki kortini.“Bw Mogikoyo amenishtaki kortini. Mimi ni mtu nisiye na ufahamu wa sheria. Mimi ni Mhandisi na kamwe singelipendelea kuendelea na kesi kama angenilipa,” Bw Oanda alimweleza hakimu mkuu Francis Andayi.

Wakili adai harudishi pesa alizotumiwa na Mungu – Taifa Leo
Christopher Onunga Oanda mlalamishi katika kesi dhidi ya Mogikoyo…Picha/RICHARD MUNGUTI

“Hii ni pesa kidogo sana kwako Bw Mogikoyo ikitiliwa maanani umekuwa wakili kwa miaka mingi na tajriba yako iko juu,” Bw Andayi alimweleza huku akiongeza kumshauri, “lipa pesa hizi uwacha kuharibu muda mwingi kortini.”Kwake Bw Oanda hakimu pia alimshauri awe na moyo wa kusamehe kwa vile muda mwingi utapotezwa waking’ang’ania pesa kidogo ambazo anaweza kuzipata kwa muda usio mrefu.

“Mbona usikubali kulipwa Sh1.5milioni na Mogikoyo,” Bw Andayi alimwuliza mlalamishi.Mhandisi Oanda alijibu na kusema , “Mimi nilimsamehe kitambo. Ni yeye wakili huyu wangu katika kesi nyingine alishangaza Pasta na Wazee wa Kanisa alipokataa kurudisha pesa zangu.

Najua neno la Mungu lasema nisiposamehe sitasamehemewa.”Wote wawili walieleza korti wangelipenda kusuluhisha mzozo baina yao nje ya mahakama na afisa atakayeteuliwa na mahakama atakayeelewa na masuala nyeti ya tofauti zao.Bw Andayi alisitisha Bw Mogikoyo kusomewa mashtaka matatu hadi ripoti ya mpatanishi iwasilishwe kortini Septemba 29 2021.

Akisimulia kilichojiri Bw Oanda alisema “ningelipenda mpatanishi huru ateuliwe na mahakama kusuluhisha kesi hii iliyoanza kusikizwa na Pasta na Wazee wa Kanisa tunakoshiriki mimi na Mogikoyo.”Lakini alisema hawakufaulu kuafikiana.

Hata hivyo alisema angelipenda waafikiane na wakili wake anayemwakilisha katika masuala kadhaa.Bw Oanda alisema katika mojawapo ya vikao vya kusaka suluhu, Bw Mogikoyo aliwaambia wahusika, “hawezi rudisha pesa hizo kwa vile alitumiwa na Mungu.”

Maungamo hayo ya Bw Oanda yalifanya hakimu kuangua kicheko pamoja na wote waliokuwa mahakamani.Hakimu aliwauliza wote Mabw Mogikoyo na Oanda ikiwa wangelipenda kusuluhisha kesi hiyo nje ya mahakama.Walikubali kusikizana na kumaliza mzozo nje ya mahakama.

“Je wewe Bw Oanda umewahi sikia neno la Mungu linalosema mmoja anapasa kusamehe mwingine,” Bw Andayi alimwuliza.“Ndio,” Bw Oanda alijibu na kuongeza kusema ,”ninalijua neno hilo na tayari nimemsamehe Bw Mogikoyo. Mimi,Bw Mogikoyo na wakili Nyabenga Mose ni Wazee wa Kanisa na kila wakati tunahimizwa tusameheane.”

Bw Oanda alisema alianza kusaka suluhu kwa kumtuma mkewe kujadiliana na mkewe wakili huyo ili wakwepe kupelekana kortini.Bw Mogikoyo pia alieleza korti angelipenda kesi hiyo isuluhishwe nje ya mahakama.“Kwa vile Mogikoyo na Oanda wamekubaliana watasuluhisha kesi hii nje ya korti nitawapa fursa waikamilishe nje ya korti,” Bw Andayi.

Endapo hawataafikia mahakama ilisema haitakuwa na budi ila kuendelea na kesi dhidi ya wakili huyo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending