Connect with us

General News

Wakongwe waliopewa kadi za NHIF hawajaweza kupata huduma za afya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakongwe waliopewa kadi za NHIF hawajaweza kupata huduma za afya – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Wakongwe waliopewa kadi za NHIF hawajaweza kupata huduma za afya

MNAMO 2018 serikali ya Kenya ilianza kutekeleza mpango wa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum katika jamii, maarufu kama Inua Jamii, kupitia ruzuku ya Sh2,000 kila mwezi.

Chini ya mpango huo, serikali kuu pia iliahidi kugharamia huduma za matibabu kwa wakongwe wenye umri wa miaka 70 kwenda juu, kupitia Bima ya Kitaifa ya Matibabu (NHIF).

Lakini tangu wakati huo wakongwe waliopewa kadi za NHIF hawajaweza kupata huduma za afya katika hospitali mbalimbali kwani serikali haijatuma pesa za bima hiyo.

Serikali isije ikasahau zaidi ya wakongwe 523,000 ambao 2018 walisajiliwa kwa mpango huu wa afya bila malipo.

Bado wanateseka kwani wengi wao hawawezi kumudu gharama zozote za matibabu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending