Connect with us

General News

Wakuzaji kahawa wajipatia soko Korea Kusini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakuzaji kahawa wajipatia soko Korea Kusini – Taifa Leo

Wakuzaji kahawa wajipatia soko Korea Kusini

NA VITALIS KIMUTAI

BAADA ya wakulima wa kahawa Kaunti ya Kericho kuuza tani 134.4 za kahawa moja kwa moja Korea Kusini, chama kimoja cha ushirika katika kaunti hiyo kimepata soko zaidi ya zao hilo nchini humo.

Chama cha Ushirika cha Kipkelion District Cooperative Union kinatarajiwa kuuza tani 40 za kahawa katika taifa hilo la bara Asia.

Wiki jana, Gavana wa Kericho Pauli Chepkwony alizindua usafirishaji wa shehena ya kwanza ya kahawa yenye thamani ya Sh110 milioni kuuzwa nchini Korea Kusini.

Jumla ya wakulima 9,852 katika kaunti za Kericho, Bomet na Nandi watafaidika na uuzaji huo wa moja kwa moja.

Kahawa hiyo ilisafirishwa baada ya chama hicho cha ushirika kupata soko katika kampuni ya Good Beans mnamo Julai mwaka jana.

Chama hicho kilikuwa kimeshiriki katika maonyesho ya kahawa jijini Seoul, Korea Kusini.

Kulingana na mkataba huo ambao utanufaisha wanachama wa vyama 67 vya ushirika, kilo moja ya kahawa itauzwa kwa Sh100.

“Katika kandarasi hii mpya, wakulima watasafirisha tani 40 za kahawa yenye thamani ya Sh31 milioni. Tunatarajia kuendelea kupenyeza soko la zao hili nchini Korea Kusini,” akasema Profesa Chepkwony.

Balozi wa Kenya nchini Korea Kusini Mwende Mwinzi kupitia taarifa alisema ubalozi huo utaendelea kuunga mkono sera ambazo zitapiga jeki uuzaji wa mazao ya Kenya nchini humo.

“Mpango huo unaonyesha kuwa serikali imejitolea kuwasaidia wakulima kupata faida. Hii ndio maana tumechuma Sh110 milioni na kuna oda nyingine ya thamani ya Sh31 milioni,” akathibitisha Bi Mwinzi.

“Usafirishaji wa shehena ya ka –

hawa ni kazi kubwa… hii ni siku muhimu kwa wakulima wa kahawa na haswa sekta yote ya kilimo nchini Kenya,” akasema Bi Mwinzi.

Shehena hiyo ilisafirishwa hadi Mombasa kupitia reli ya kisasa (SGR).

Ufanisi huo wa uuzaji wa kahawa moja kwa moja katika mataifa ya kigeni umewezeshwa na mageuzi katika sekta ya kahawa yaliyoanzishwa na serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

Jopokazi lililoongozwa na Profesa Joseph Keiyah lilipendekeza mageuzi hayo.

Serikali ya Kaunti ya Kericho imeajiri maafisa wa kilimo nyan – jani katika wadi zote sita ambako kunakuzwa kahawa kama hatua ya kuimarisha uzalishaji wa kahawa.

Kupitia utunzaji mzuri, uzalishaji unatarajiwa kupanda kutoka kilo 1 hadi 5 kwa mti mmoja hadi kilo 10 kwa mti mmoja ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo.

“Ili kuwawezesha wakuli – ma kuongeza thamani kwa zao lao, serikali ya kaunti imenunua mashine maalum ya kusaga kahawa. Mashine hizo zimesambazwa katika vituo vinavyosimamiwa na vyama vidogo vya ushirika.

Tumesaidia zaidi ya vyama 20 vya ushirika chini ya mpango huu wa kuongeza thamani,” akasema gavana Chepkwony.

Chama cha Ushirika cha Kipkelion kinatarajiwa kuuza tani 40 zaidi za kahawa katika taifa hilo la bara Asia na kuchuma Sh31m