Connect with us

General News

Walimu wakuu Nyandarua kushtakiwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Walimu wakuu Nyandarua kushtakiwa – Taifa Leo

Fujo shuleni: Walimu wakuu Nyandarua kushtakiwa

Na KENYA NEWS AGENCY

MKURUGENZI wa Elimu Kaunti ya Nyandarua Philip Wambua amewaonya walimu wakuu kwamba watashtakiwa ikiwa washindwa kudhibiti visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi katika shule zao.

Akiwahutubia walimu wakuu kutoka kaunti ndogo za Nyandaraua Kaskazini na Aberdares katika Shule ya Upili ya Baari, Wambua alisema walimu wakuu watawajibikia uharibifu wa mali kutoka na utepetevu wao.

“Ikijulikana kwamba wanafuynzi waliibua malalamishi na ukafeli kuchukua hatua kisha wakazua fujo na uharibifu wa mali, utashtakiwa kwa kutenda uhalifu,” Wambua akasema.

Mkurugenzi huyo wa elimu aliwahimiza walimu wakuu na manaibu wao kufuatilia kwa makini yale yanayotendeka katika shule zao kila. Pia aliwataka kuishi ndani ya shule ili waweze kuzima malalamishi kutoka kwa wanafunzi hao haraka iwezekanavyo.

Mbunge wa Ndaragua Jeremiah Kioni ambaye alikuwa mgeni mheshimiwa katika mkutano huo alilalamika kuwa baadhi ya wanafunzi werevu kutoka eneo bunge lake wanahamishwa hadi Nairobi.

“Lengo la wanaowahamisha wanafunzi hawa huwa ni kuvutia pesa kutoka kwa wadhamini kutoka ng’ambo. Hii sio haki na mwenendo kama huu unafaa kukomeshwa kabisa,” Bw Kioni akasema.

Mbunge huyo alisema baadhi ya wanafunzi wanaohamishwa hadi shule za Nairobi baadaye huishia kuandikisha matokeo mabaya katika mitihani ya kitaifa. “Walimu ambao waliwafunza wanafunzi hawa hushangaa baadaye kuarifiwa kuwa wanafunzi warevu wamehamishwa hadi Nairobi hawawezi kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiingereza,” akasema Bi Kioni.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending