– Walinzi hao wameripotiwa kukutwa na virusi hivyo wakati wa mkutano wa kisiasa ulioandaliwa na Rais Trump
– Kwa sasa walinzi wote wa Trump wametakiwa kujitenga baada ya wenzao kupatikana na virusi hivyo hatari
– Kufikia sasa, Marekani imerekodi visa milioni 2.3 vya maambukizi ya virusi vya corona na zaidi ya vifo 121, 000 vimeripotiwa
Walinzi wawili wa Rais wa Marekani Donald Trump wamepatikana na virusi vya ugonjwa wa corona, wenzao wengine wametakiwa kujiweka karantini.
Imeripotiwa kuwa walinzi hao walikutwa na virusi hivyo wakati Rais Trump alifanya mkutano wa kisiasa katika mji ambao umeathirika pakubwa na ugonjwa huo.
Imeripotiwa kuwa raia waliohudhuria mkutano wa kisiasa wa Tusla hawakuhitajika kuvaa maski wala kuzingatia masharti ya kutokaribiana lakini cha muhimu ilikuwa ni kupimwa kiwango cha joto mwilini.
Kufikia sasa, Marekani imerekodi visa milioni 2.3 vya maambukizi ya virusi vya corona na zaidi ya vifo 121, 000 vimeripotiwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.