Connect with us

General News

Walioathiriwa na nzige waanza kupokea fidia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Walioathiriwa na nzige waanza kupokea fidia – Taifa Leo

Walioathiriwa na nzige waanza kupokea fidia

SAMMY LUTTA NA ALEX NJERU

SERIKALI ya kitaifa imekumbatia mpango wa kuwafidia wakulima ambao mimea yao iliharibiwa miaka miwili iliyopita kutokana na uvamizi wa nzige.

Mpango huo ambao unafadhiliwa na pesa kutoka Benki ya Dunia unalenga kuwanufaisha wakulima kutoka kaunti 15 ambazo ziliathirika sana na uvamizi wa wadudu hao hatari mnamo 2019.

Katika Kaunti ya Turkana, wakazi katika wadi 10 watapokea Sh36 milioni, baada ya mimea yao iliyokuwa katika ekari 15,000 za ardhi, kuharibiwa na kuathiri zaidi maisha yao ikizingatiwa wao ni wafugaji wa kuhamahama.

Kwa mujibu wa wakuu wa kaunti hiyo, uvamizi huo uliwarejesha nyuma kwa kuwa walikuwa wakishiriki kilimo cha unyunyuziaji mashamba maji kwa sababu ya ukame katika eneo hilo.

Waziri wa Kilimo na Ufugaji katika kaunti hiyo, Bw George Emoru, alisema kuwa wametambua wadi 10 ambazo ziliathirika zaidi na tayari wamebuni kamati ambayo itahakikisha kuwa pesa hizo zinatolewa bila mapendeleo yoyote.

Wakazi watakaonufaika watatoka kwenye wadi za Kapedo/ Napeitom, Lokori/Kochodin, Lobei/Kotaruk, Lokiriama/Lorengkipi, Letea, Kalapata, Kaeris, Kerio, Kaputir na Kanamkemer.

Bw Emoru aliongeza kuwa fidia hiyo itahakikisha waliopata hasara kutokana na uvamizi wa nzige wanarejelea maisha yao ya hapo awali na kuendeleza kilimo cha mimea badala ya kumakinikia ufugaji pekee.

“Fidia hiyo ni ya kuhakikisha kuwa wakulima na wafugaji wanarejelea maisha yao kama hapo awali. Ingawa fedha hizo huenda zisitoshe kiwango cha faida wangepata kutokana na kilimo, itawapunguzia hasara na kuwashaajisha warejelee kilimo cha unyunyuziaji mashamba maji badala ya ufugaji tu,” akasema Bw Emoru.

Naye afisa mkuu anayehusika na ufugaji, Bw Abdullahi Yusuf, alisema lengo lao ni kuhakikisha kuwa kila familia inajitosheleza kwa chakula na akatoa wito watakaopokea pesa hizo kuzitumia kwa miradi yenye faida.

Bw Yusuf alisema Turkana ni kati ya kaunti ambazo ziliathirika zaidi na uvamizi wa nzige na kwamba serikali ya gatuzi hilo imekuwa likishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Kilimo na Chakula Duniani (FAO) kuwasaidia wakazi kurejelea kilimo.

Katika Kaunti ya Tharaka-Nithi, wakulima ambao mimea yao iliharibiwa na nzige hao, wamepokea Sh2.2 milioni.

Gavana Muthomi Njuki aliwataka wakulima kutumia vyema pesa hizo baada ya kuzigawa kwa makundi 20 ya wakulima katika lokesheni za Gatue, Maragwa, Kanjoro na Kathangacini.

Hasa, aliwataka walionufaika na pesa hizo kununua vyakula na mbegu za msimu unaokuja wa upanzi.

Pia aliahidi kuwa serikali yake inalenga kuwapa wakulima dawa za kunyunyuzia nzige iwapo uvamizi mwingine utatokea.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending