Connect with us

General News

Waliopewa zabuni ya kufufua Mumias hatarini kutupwa jela – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waliopewa zabuni ya kufufua Mumias hatarini kutupwa jela – Taifa Leo

Waliopewa zabuni ya kufufua Mumias hatarini kutupwa jela

Na SAM KIPLAGAT

MAAFISA wakuu wa kampuni ya Uganda iliyoshinda zabuni ya kufufua kiwanda cha sukari cha Mumias huenda wakasukumwa jela kwa kukaidi agizo la mahakama wakitaka harakati za kuzindua kiwanda hicho kinachokumbwa na matatizo zisitishwe.

Kampuni ya Tumaz & Tumaz Enteprises iliwasilisha kesi katika mahakama kuu Alhamisi wiki hii ikimlaumu Bw Sarbjit Rai mmiliki wa kampuni ya Uganda ya Sarrai Group kwa kukaidi agizo la mahakama.

Katika kesi hiyo Tumaz imelaumu kampuni hiyo ya Uganda , Bw Rakesh Kumar Bvats na meneja aliyeteuliwa na KCB Group Bw Ponangipalli Venkata Ramana Rao kwa kukaidi agizo la mahakama.

Agizo hilo lilisimamisha kuteuliwa kwa wasimamizi wapya wa kiwanda hiki cha sukari cha Mumias (MSC).

MKATABA

Kwa mujibu wa mkataba uliopo, kampuni itakayoteuliwa kusimamia MSC itasalia usukani kwa miaka 20.

Mnamo Desemba 29,2021 kampuni ya Tumaz & Tumaz iliwasilisha kesi ikidai zoezi la kuteua kampuni ya kukifufua kiwanda cha MSC ilikumbwa na ufisadi.

Wakili Julius Mwale , anayewakilisha Tumaz aliilaumu kampuni ya Sarrai Group inayohusishwa na familia tajiri ya Rai kwa kuanza kazi ya kufufua kiwanda cha MSC mnamo Desemba 24, 2021.

Kati ya kazi ambazo Sarrai ilianza ni kufanya mkutano na maafisa wakuu wa kampuni ya umeme ya Kenya Power kurejesha stima katika kiwanda hicho cha sukari.Vile vile, kampuni hiyo ya Uganda imekuwa ikifanya mashauriano na Wahandisi kuweka mikakati ya kuanza usagaji wa sukari tena.

Pia Sarrai imeanza kuwaajiri wafanyakazi upya.Tumaz imedai kwamba mashauri yanayoendelea na ajira ya wafanyakazi inakaidi agizo hilo la mahakama.

Sarrai Group iliwasilisha kesi katika mahakama kuu kubatilisha uamuzi huo wa kuizima isianze kazi.Sarrai iliwasilisha ushahidi mnamo Januari 3,2022 ukionyesha matinga tinga yakilima shamba la Mumias.