Connect with us

General News

Walivyong’aa katika mazingira yenye changamoto tele – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Walivyong’aa katika mazingira yenye changamoto tele – Taifa Leo

#KCPE2021: Walivyong’aa katika mazingira yenye changamoto tele

NA WAANDISHI WETU

WATAHINIWA waliotia fora kwenye Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) wa Mwaka 2021, walimu na wazazi wameelezea siri walizotumia kupata matokeo bora kwenye mtihani huo licha ya changamoto tele zilizoambatana na janga la corona.

Watahiniwa wa KCPE mwaka jana walilazimika kukaa nyumbani kwa zaidi ya miezi kumi shule zilipofungwa kuzuia kusambaa kwa corona.

Wengi walisema, walilazimika kutia bidii ya ziada na kuomba Mungu huku wakishukuru walimu na wazazi kwa ushirikiano wao.

Msichana Mbugua Sharon Wairimu Muteti, 14, aliyeibuka wa tano kote nchini, anasema alitia bidii akilenga kujiunga na Shule ya Upili ya Wasichana ya Alliance. Mamake, Bi Serah Watiri, alimtaja bintiye kuwa mwadilifu na mwenye bidii. Mwanadada huyo alikuwa akisomea katika Shule ya Msingi ya Emmanuel, eneo la Kangari, Kaunti ya Murang’a ambayo ilipata alama za wastani 400.3.

Kwa Sheila Chepkoech, aliyekuwa mwanafunzi katika Shule ya Ansam Pioneer School, wadi ya Merigi, Kaunti ya Bomet, ilikuwa baraka kutoka kwa Mungu kuzoa alama 389 kwenye mtihani huo.

“Ninamshukuru sana Mungu, wazazi wangu na walimu kwa matokeo hayo. Ninaahidi kutia bidii kwenye shule ya upili nitakayojiunga nayo ili kutimiza ndoto yangu ya kuwa daktari.” Mwalimu wake, Collins Rotich, alikiri kwamba, mwanafunzi huyo alipata alama nyingi kuliko matarajio ya wengi.

Nomi Chepng’etich aliongoza katika shule hiyo mpya baada ya kuzoa alama 404. Wanafunzi hao ni wa kwanza katika shule hiyo kufanya mtihani wa KCPE. “Nina furaha sana kuibuka bora kwenye mtihani huu. Mafanikio haya yanayokana na maombi, msaada kutoka kwa wazazi, walimu na wanafunzi wenzangu,” akasema.

Katika Kaunti ya Kirinyaga, Shule ya Msingi ya St Agnes ilipata alama ya wastani ya 372.7, ikiibuka shule bora zaidi ya msingi ya umma kwenye mtihani huo katika Kaunti ya Kirinyaga.

Watahiniwa wote katika shule hiyo walifaulu kupata alama zitakazowawezeasha kujiunga na shule bora za upili.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bi Felista Nyokabi, wanafunzi 19 walizoa alama 400 kwenda juu huku 42 kati yao wakizoa alama 380 na zaidi. Shule hiyo ndiyo ilitoa mwanafunzi bora zaidi katika eneo hilo, Susan Njeri, aliyezoa alama 418 kati ya 500. Alifuatwa na Natalie Wanjiru, aliyezoa alama 417. Mtahiniwa mwingine, Njenga Mercy Muthoni, alizoa alama 412.

“Tulikuwa tukikabiliwa na changamoto nyingi sana japo hilo halikutuzuia kushinda shule za msingi za kibinafsi na umma katika kaunti hii,” akasema Bi Ng’ang’a. Mwalimu huyo alitaja mafanikio hayo kuchangiwa na maombi na bidii miongoni mwa wanafunzi.

Na George Munene, Mwangi Muiruri, Vitalis Kimutai, Stanley Ngotho, Glorah Koech, Fred Kibor na KNA