Connect with us

General News

Waluke aruka Ruto, aingia Jubilee – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waluke aruka Ruto, aingia Jubilee – Taifa Leo

Waluke aruka Ruto, aingia Jubilee

NA CECIL ODONGO

CHAMA cha Jubilee kinaendelea kushuhudia ufufuo mkubwa na jana kilivuna baada ya mbunge wa Sirisia John Waluke ambaye amekuwa UDA kurejea nyumbani.

Waluke, ambaye ni mwandani wa Naibu Rais Dkt William Ruto na mkosoaji mkuu wa serikali alikuwa kati ya wanasiasa waliopokelewa katika makao ya Jubilee na mbunge wa Kieni Kanini Kega.

Chama hicho kipo kwenye vuguvugu la Azimio la Umoja ambalo kuwa watamuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga. Ingawa alichaguliwa kwa tiketi ya Jubilee

baada ya kuhudumu chini ya ODM muhula wake wa kwanza, Bw Waluke kwa muda wa miaka mitano amekuwa akimuunga Dkt Ruto na ni kati ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiandamana naye kwenye ziara yake eneo hilo.

Bw Waluke pamoja na mfanyabiashara Grace Wakhungu wapo nje kwa dhamana baada ya kutozwa faini ya Sh1 bilioni moja kutokana na kashfa ya mahindi mwaka uliopita.

Kando na Bw Waluke, msanii Kevin Bahati pia alijiunga na chama hicho huku akilenga kiti cha ubunge wa Starehe.