Connect with us

General News

Wamalwa amgonga Ruto kukejeli chama chake cha ‘Mbolea’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wamalwa amgonga Ruto kukejeli chama chake cha ‘Mbolea’ – Taifa Leo

Wamalwa amgonga Ruto kukejeli chama chake cha ‘Mbolea’

Na BRIAN OJAMAA

WAZIRI wa Ulinzi, Eugene Wamalwa, amemkashifu vikali Naibu Rais William Ruto kwa kuvipuuza vyama vipya vya kisiasa huku uchaguzi mkuu wa Agosti unapoedelea kukaribia.

Akiwahutubia wakazi wa Bungoma katika Shule ya Upili ya Sipala, eneobunge la Webuye Mashariki mnamo Jumatatu, Bw Wamalwa alisema kuwa Kenya ni nchi ya kidemokrasia, ambapo kila chama kinapaswa kuruhusiwa kuendeleza sera zake bila pingamizi zozote.

Waziri huyo, ambaye alikuwa ameandamana na mwenzake wa Mazingira, Keriako Tobiko, pia alimkosoa Dkt Ruto kwa kuwashurutisha wenyeji wa eneo hilo kujiunga na chama chake cha UDA.

Bw Wamalwa, ambaye majuzi alibuni chama cha DAP-Kenya, alisema kitapata umaarufu sana katika eneo hilo kwani tayari wenyeji washaanza kukikumbatia.

“Tunataka kampeni za amani na heshima katika eneo la Magharibi na maeneo mengine nchini uchaguzi mkuu unapoendelea kukaribia,” akasema.

Bw Wamalwa alisema kuwa kila mwaniaji urais anapaswa kuruhusiwa kuzuru katika kila sehemu nchini kufanya kampeni zake bila kuingiliwa.

“Tunataka kila mwanasiasa kuja katika eneo la Magharibi na kuuza ajenda zake. Hata hivyo, anafaa kuendesha kampeni zake kwa njia ya amani. Hapaswi kuwadharau wenyeji,” akasema.

Alisema wale wanaotafuta kura katika eneo hilo hawapaswi kutumia matusi au lugha chafu kuwarai wenyeji kuwaunga mkono.

“Nimemsikia Dkt Ruto akiwaambia wenyeji kwamba wanapaswa kukataa vyama vyetu kwani ni vya kikabila. Alisema wanapaswa kujiunga na UDA pekee. Namwambia kuzingatia hekima anapofanya kampeni zake,” akasema.

Alieleza kuwa wale wanaokitaja chama hicho kuwa “cha kijiji” watashangazwa na idadi ya viti kitakavyoshinda ifikapo Agosti.

“Ningetaka kuwaambia wenye shaka kwamba tulipoanzisha chama cha New Ford-Kenya miaka ya hapo nyuma, kilikuwa chama kidogo sana. Hivyo, wasitudharau kwani huu ni mwanzo tu,” akasema.

Akaongeza: “Tulianzisha New Ford-Kenya tukiwa na Dkt Ruto, wakati yeye alikuwa na chama cha URP huku Rais Uhuru Kenyatta akiwa na TNA. Hata hivyo, kilikua na kuwa chama kikubwa kiasi cha mmoja wa wawaniaji wake kuibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro cha ugavana katika Kaunti ya Bungoma. Kwa sasa, Bw Ken Lusaka ndiye Spika wa Seneti.”

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending