Connect with us

General News

Wanabadminton wa Kenya furaha tele kuruhusiwa kucheza Jumuiya Madola licha ya migogoro – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanabadminton wa Kenya furaha tele kuruhusiwa kucheza Jumuiya Madola licha ya migogoro – Taifa Leo

Wanabadminton wa Kenya furaha tele kuruhusiwa kucheza Jumuiya Madola licha ya migogoro

Na GEOFFREY ANENE

WACHEZAJI wa badminton nchini wana sababu ya kutabasamu tena baada ya Shirikisho la Badminton Duniani (BWF) kuruhusu Kenya kushiriki michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Birmingham, Uingereza mnamo Julai 28 hadi Agosti 8.

Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) ilifanikiwa katika ombi lake kwa BWF kuruhusu wachezaji wa Kenya wapewe fursa.

Wakenya walikuwa wamezuiwa kushiriki michezo hiyo baada ya Shirikisho la Badminton Kenya kupigwa marufuku na BWF kwa sababu ya migogoro ya uongozi isiyoisha.

“Uamuzi ulifanywa na BWF kuruhusu wachezaji wa Kenya kucheza chini ya bendera ya Kenya na tunafurahi kuweka wazi tangazo hilo kwa umma zinaposalia siku 140 michezo ya Jumuiya ya Madola,” alisema katibu wa NOC-K, Francis Mutuku, Ijumaa.

“Tunashukuru BWF kwa kuwa na moyo wa Olimpiki. Wachezaji wote watapewa fursa sawa kushindana. Matumaini yetu ni kuwa watapata fursa ya kushiriki michezo hiyo bila ya kuzuiwa na sarakasi zinazoendelea nje ya wanja,” alisema Mutuku.

Mshindi wa medali ya shaba ya michezo ya Afrika 2019 Mercy Joseph Mwethya na nahodha wa timu ya taifa John Wanyoike ni baadhi ya wachezaji walioelezea furaha yao kukubaliwa kupewa fursa ya kuwania tiketi za michezo ya Jumuiya ya Madola na mashindano yenyewe wakifuzu.

“Tunashukuru sana NOC-K kwa juhudi zao ambazo zimezaa matunda. Nasubiri kwa hamu kuwakilisha taifa kwa michezo ya Jumuiya ya Madola,” alisema.

Wanyoike anatumai kupata tiketi ya kuwakilisha Kenya katika michezo hiyo kwa mara ya kwanza kabisa.

“Nimejaribu mara mbili kufuzu kushiriki michezo ya Jumuiya ya Madola bila mafanikio. Kuna wakati mmoja nilimaliza mashindano ya kufuzu katika nafasi ya pili na mshindi pekee ndiye alikuwa ananyakua tiketi. Kupata fursa hii na habari hizi ni fursa nzuri sana. Nimekuwa nikifanya mazoezi nikitumai kupata fursa hii. Natumai kushiriki mashindano ya kufuzu na kujikatia tiketi ya kupeperusha bendera ya Kenya,” alisema Wanyoike.

Mashindano mawili ya kitaifa yataandaliwa kuchagua timu ya taifa ya wachezaji wanane wa kike na wanane wa kiume watakaohudhuria mashindano matatu ya kimataifa ili kuingia michezo ya Jumuiya ya Madola.

Kufikia sasa, timu za Kenya zinazoelekea Birmingham ni wanaraga wa Kenya Shujaa, timu za mpira wa vikapu za kinadada na wanaume za wachezaji watatu kila upande (3×3) na timu ya kinadada ya mpira wa magongo.