Connect with us

General News

Wanabiashara wa miraa wakashifu serikali kwa kukosa kuwatengea hela – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanabiashara wa miraa wakashifu serikali kwa kukosa kuwatengea hela – Taifa Leo

Wanabiashara wa miraa wakashifu serikali kwa kukosa kuwatengea hela

NA DAVID MUCHUI

MUUNGANO wa wafanyabiashara ya miraa umeshutumu serikali kwa kutelekeza sekta hiyo na hata kukosa kutenga fedha kwa ajili ya biashara hiyo katika mwaka huu wa fedha.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Miraa Nyambene, Kimathi Munjuri, alise – ma kuwa serikali imeshindwa kutimiza ahadi kadhaa za kus – hughulikia ukosefu wa soko la miraa nchini Somalia, miaka mitatu sasa.

Kadhalika, alimshutumu Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i kwa kutoa matumaini ya uongo kwa wafanyabiashara wa miraa alipoahidi kurekebisha mzozo wa soko la Somalia ndani ya siku 10.

“Ofisi ya Rais iliahidi kushughulikia suala la soko la Somalia ndani ya siku 10. Ni miaka mitatu sasa tangu ahadi itolewe. Kadhalika Dkt Matiang’i aliahidi ku – unda kamati ya mawaziri kushughulikia masuala ya miraa. Bado hatujaona manufaa yoyote ya ahadi hii,” akasema Bw Munjuri.