Connect with us

General News

Wanafunzi 302 ndani kwa uchomaji shule – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanafunzi 302 ndani kwa uchomaji shule – Taifa Leo

Wanafunzi 302 ndani kwa uchomaji shule

Na FAITH NYAMAI

RIPOTI ya Wizara ya Elimu inaonyesha kuwa wanafunzi 302 walikamatwa kwa kujihusisha na visa vya kuteketeza mabweni ya shule mbalimbali vinavyoendelea kuripotiwa nchini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanafunzi 126 walikamatwa kati ya Novemba 1 na Novemba 11 huku wengine wikinyakwa kati ya Januari 1 na Oktoba 30 na vyombo vya sheria.

Kati ya idadi yote ya wanafunzi waliokamatwa, 41 washafikishwa kortini huku wengine kesi zao zikisikizwa na kamati ya nidhamu ya shule zao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotiwa saini na Waziri wa Elimu, Prof George Magoha, matumizi ya dawa za kulevya, msongamano madarasani na kwenye mabweni, na kutibuka kwa mawasiliano kati ya wanafunzi na walimu ni baadhi ya sababu zilizochangia migomo mingi shuleni.

“Kamati za ujasusi na usalama katika kaunti mbalimbali zimeamrishwa ziandae mikutano na wadau mbalimbali kwenye sekta ya elimu ili suala hili la migomo shuleni lipate ufumbuzi,” akasema Prof Magoha kwenye ripoti hiyo.

Masuala mengine ambayo yamechangia ongezeko la migomo shuleni ni kalenda ya masomo ambayo inawapa wanafunzi muda mfupi sana wa kupumzika na pia imepunguza michezo shuleni.

Vilevile katika shule nyingi hakuna huduma za mwongozo na ushauri nasaha.

“Tawala za shule nyingi ni dhalimu na hukandamiza uhuru wa wanafunzi ilhali wakiwa nyumbani, wazazi wao huwaruhusu watende mambo jinsi watakavyo. Hii ni kati ya kisababishi kikuu cha mgomo wa wanafunzi shuleni,” ikaongeza ripoti hiyo.

Profesa Magoha pia amelaumu athari hasi ya vyombo vya habari hasa runinga na mitandao ya kijamii, akisema imekuwa ikisifia ghasia.

Wanafunzi wengi huwa wana uwezo wa kupata habari kuhusu matukio mbalimbali kitaifa na kimataifa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa wengi huwa na simu nyumbani.

Aidha waziri huyo pia aliilaumu familia na jamii kwa kuchangia kupotea kwa maadili miongoni mwa wanafunzi akisema kuwa wazazi wengi hawafuatilii mienendo ya watoto wao hata wakati shule zimefungwa.

“Iwapo wazazi hasa baba akikosa kuodhirisha uongozi nyumbani, basi kutakuwa na shida. Hiyo ndiyo maana migomo mingi imekuwa ikitokea kati shule za wavulana,” akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending