Connect with us

General News

Wanafunzi wengi hawamalizi elimu ya sekondari – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanafunzi wengi hawamalizi elimu ya sekondari – Taifa Leo

Ripoti: Wanafunzi wengi hawamalizi elimu ya sekondari

NA DAVID MUCHUNGUH

MWANAFUNZI mmoja kati ya watatu katika shule za upili huwa hamalizi masomo na wataendelea kuacha shule.

Hii ni licha ya fedha nyingi zinazotengwa kuhakikisha wanafunzi zote wanaomaliza shule za msingi wamejiunga na zile za upili.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuhusu hatua zilizopigwa na mataifa mbalimbali katika elimu, imebainika karibu asilimia 35 ya wanafunzi hawatamaliza masomo ya shule za upili kufikia mwaka 2030.

Hili ni bila kuzingatia athari za janga la virusi vya corona, ambalo limeathiri sana sekta ya elimu.

Hilo linamaanisha kuwa kati ya wanafunzi 1.4 milioni walio katika Gredi ya Tano na wanaotarajiwa kujiunga na shule ya upili ya kiwango cha chini mwaka ujao, karibu wanafunzi 500,000 hawatamaliza masomo yao katika shule ya upili ya kiwango cha juu mwaka 2028.

Licha ya hayo, hilo litakuwa hatua kubwa kwani ni asilimia 47.7 pekee ya wanafunzi waliomaliza masomo yao ya shule ya upili mnamo 2015.

Ripoti zinaonyesha kuwa maelfu ya wanafunzi hukosa kujiunga na shule za upili kila mwaka kutokana na sababu tofauti.