Connect with us

General News

Wanajeshi wa KDF waua wapiganaji wanne wa al-Shabaab msituni Boni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanajeshi wa KDF waua wapiganaji wanne wa al-Shabaab msituni Boni – Taifa Leo

Wanajeshi wa KDF waua wapiganaji wanne wa al-Shabaab msituni Boni

NA KALUME KAZUNGU

WANAJESHI wa Kenya (KDF) wamewaua wapiganaji wanne wa al-Shabaab na kuwajeruhi wengine kadhaa katika eneo la Sarira lililoko katika msitu wa Boni, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Ofisi ya Masuala ya Mpangilio wa Mawasiliano ya Jeshi la KDF ilithibiisha kuwa mauaji ya wanamgambo hao wanne yalitekelezwa Jumamosi majira ya saa moja unusu asubuhi.

Kulingana na ofisi hiyo ya mawasiliano ya KDF, magaidi hao walikuwa kwenye harakati za kuvuka mpaka wa Kenya na Somalia ili kuingia Lamu kupitia eneo hilo la Sarira lakini makabiliano makali yakazuka kati yao na KDF,hivyo magaidi hao kuuawa wanne papo hapo ilhali wengine wengi wakifaulu kutoroka na majeraha ya risasi.

Hata hivyo hakuna mwanajeshi hata mmoja wa KDF aliyeuawa au kuijeruhiwa kwenye makabiliano hayo.

Kufuatia tukio hilo, usalama umeimarishwa vilivyo kote Lamu, hasa maeneo yaliyokaribiana na msitu wa Boni na pia yale ya mpakani mwa Kenya na Somalia wakati msako mkali wa kuwatafuta magaidi zaidi, ikiwemo wale waliotoroka na majeraha makali ya risasi ukiendelea.

“Tumezidisha doria za walinda usalama wetu wakati tukiwasaka magaidi na kuwamaliza. Cha msingi ni wananchi kuendelea kushirikiana nasi ili kukabiliana na kuwashinda hawa magaidi,” ikasema ripoti ya KDF ambayo Taifa Leo iliona.

Mauaji ya magaidi wanne wa Al-Shabaab Jumamosi aidha ilipokelewa vyema na wananchi wa Lamu,hasa wale wa vijiji vya msitu wa Boni na wale wa mpakani mwa Kenya na Somalia.

Ali Abdi ambaye ni mkazi wa msitu wa Boni alisema kuuawa kwa al-Shabaab hao ni dhahiri kwamba operesheni inayoendelea kwenye msitu wa Boni inazaa matunda.

“Tumefurahia kusikia kwamba wapiganaji wanne wa al-Shabaab wameangamizwa Sarira. Sisi tutaendelea kushirikiana na maafisa wa usalama wanaoendeleza operesheni ya Linda Boni ili kuona kwamba ugaidi unamalizwa eneo hili. Furaha yetu ni kuishi kwa amani, raha mstarehe,” akasema Bw Abdi.

Mauaji hayo ya al-Shabaab wanne Jumamosi yanajiri wiki mbili tu baada ya mtu mmoja kujeruhiwa na wengine sita wakiponea bila majeraha pale gari walimokuwa wakisafiria lilipokanyaga kilipuzi cha kutegwa ardhini na kuharibika kati ya Milimani na Baure, ndani ya msitu wa Boni.

Shambulizi hilo lilitekelezwa na al-Shabaab mnamo Februari 12, 2022.

Januari 26 mwaka huu, maafisa zaidi ya watano wa mahakama walijeruhiwa pale gari walimokuwa wakisafiria kutoka eneo laKipindi kuelekea Garsen lilipomiminiwa risasi na washukiwa wa Al-Shabaab eneo la Lango la Simba, karibu na Nyongoro kwenye barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen.

Januari 23 mwaka huu, magaidi wa Al-Shabaab walivamia kambi ya ujenzi wa barabara ya kuunganisha mradi wa bandari ya Lamu (Lapsset) eneo la Kwa Omollo, ndani ya msitu wa Boni ambapo waliteketeza magari na matingatinga ya ujenzi manane.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending