[ad_1]
Wanaokosa kulipa mikopo ya Sacco kuingia CRB
NA MWANDISHI WETU
MAELFU ya Wakenya wanaokataa kulipa mikopo ya Mashirika ya Akiba na Mikopo (Sacco) huenda sasa wakajipata mashakani baada ya Bunge kuidhinisha sheria inayoshurutisha Sacco kutoa habari kwa CRB.
Sheria iliyofanyiwa Marekebisho kuhusu Mashirika ya Akiba na Mikopo ilipitishwa katika kikao cha pili cha kusikizwa Bungeni kilichofanyika Jumatano jioni.
Mswada huo unanuia kubadilisha jinsi Sacco zinavyoendesha shughuli zake. Unaambatana na Sheria kuhusu Mashirika ya Akiba na Mikopo 2008, Sheria kuhusu Mashirika ya
Benki ikiwemo Sheria kuhusu Mashirika kuhusiana na Mikopo ya Kifedha, hivyo kujumuisha sheria kuhusu usambazaji wa habari katika mfumo mmoja.
Kwa sasa, Sacco zinahitajika kuchapisha habari njema kuhusu
mikopo miongoni mwa wanachama lakini kutuma data kwa mashirika ya CRB chini ya kitengo tofauti.
Kitengo hicho kulingana na Sheria kuhusu CRB 2013, inahitaji Sacco kupata idhini kutoka kwa Benki Kuu ya Kenya (CBK) na kuomba ruhusa kutoka kwa wateja wake kabla ya kuchapisha habari kuhusu mikopo.
Mswada huo unashurutisha Sacco kutoa habari zote njema na mbaya kuhusu wateja wao kwa mashirika ya CRB yaliyoidhinishwa.
Mashirika hayo yatahitajika kutoa notisi kabla na baada ya kuorodhesha wateja wao jinsi inavyohitajika kisheria.
Next article
Siri ya mawaziri ‘wanasiasa’ kutojiuzulu viti
[ad_2]
Source link