[ad_1]
Wanaraga wa Oilers na Kabras waingia fainali ya Ligi Kuu ya Kenya Cup
Na GEOFFREY ANENE
Hatimaye Menengai Oilers imevumbua siri ya kuvuna ushindi dhidi ya KCB baada ya kupiga wanabenki hao kwa mara ya kwanza katiia kwenye Ligi Kuu ya raga (Kenya Cup) 24-17 katika nusu-fainali uwanjani Ruaraka, Jumamosi.
Mabingwa wa 2016 Kabras Sugar nao wamelima Strethmore Leos 29-9 mjini Kakamega katika nusu-fainali nyingine kwa hivyo fainali itakuwa kati ya Oilers na Kabras mnamo Machi 12.
Oilers ya kocha Gibson Weru ilikuwa imepoteza mikononi mwa wanabenki wa KCB mara saba mfululizo tangu waingie Kenya Cup msimu 2018-2019.
Kabla ya mechi, Weru alieleza Taifa Leo kuwa Oilers wamejiandaa vyema tangu msimu huu.
“Lengo letu la kwanza lilikuwa kufika nusu-fainali kwa hivyo tumetimiza lengo hilo. Sasa, tunataka kutafuta mafanikio zaidi. KCB ni timu nzuri sana na iliyojaa na wachezaji wazoefu. Itakuwa mechi ngumu. Hata hivyo, tunaamini tumeimarika sana tangu tukutane nao katika nusu-fainali mwaka jana,” alisema Weru akifichua kuwa Dalmas Chituyi yuko nje kwa sababu ya jeraha la kisugudi, Samson Onsomu (muundi), Tyson Maina (kifundo) na Timothy Omela (kupoteza fahamu baada ya kugongwa kichwa).
Bila ya wachezaji hao nyota, Oilers bado ilisumbua mabingwa hao wa 2005, 2006, 2007, 2015, 2017, 2018, 2019 na 2021.
Oilers, ambao wanakufuzia taji lao la kwanza kabisa ligini, waliongoza 12-7 wakati wa mapumziko nao Kabras waliongoza Strathmore 14-9 baada ya dakika 40 za kwanza.
Next article
Karan Patel mawindoni kumaliza nuksi Nakuru Rally
[ad_2]
Source link