Connect with us

General News

Wanasiasa wahimizwa waweke zingatio kwa sekta ya kilimo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanasiasa wahimizwa waweke zingatio kwa sekta ya kilimo – Taifa Leo

Manifesto: Wanasiasa wahimizwa waweke zingatio kwa sekta ya kilimo

NA SAMMY WAWERU

WAGOMBEA wa viti mbalimbali vya kisiasa wametakiwa kuipa kipau mbele sekta ya kilimo kwenye manifesto zao, wanapoendeleza kampeni.

Kampeni zimepamba moto nchini, wanasiasa wakijitosa nyanjani kuomba kura kuchaguliwa viti tofauti vya kisiasa.

Wakiongozwa na kinara wa Azimio, Bw Raila Odinga na mwenzake wa Kenya Kwanza, naibu wa rais, William Ruto, wanaendelea kuzuru maeneo mbalimbali nchini kusaka uungwaji mkono.

Wawili hao, ni kati ya wanaomezea mate kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022, kila mmoja akitoa ahadi chungu mzima kukomboa uchumi wa taifa.

Muungano wa wadauhusika wa kibinafsi katika shughuli za kilimo, ASNET umehimiza wanasiasa kuipa nafasi ya kwanza sekta ya kilimo, ukisisitiza itaimarika kupitia kujitolea kwa viongozi hao.

Kauli hiyo, imejiri wakati ambapo bei ya pembejeo na ya chakula cha mifugo inazidi kuwa ghali.

Tayari, baadhi ya wakulima wameacha shughuli za kilimo-ufugaji-biashara walizokumbatia kutokana na mfumko wa bei.

“Tunahimiza viongozi wanaomezea mate na kuwania viti vya kisiasa, waipe kipau mbele sekta ya kilimo kwenye manifesto zao.

“Hiyo ndiyo njia ya kipekee sekta hii itaimarika na kuboreka,” akasema Dkt Bimal Kantaria, mwenyekiti wa ASNET.

Muungano huo ulioanzishwa 2020 aidha umekuwa ukishirikiana kwa karibu na serikali, kupitia Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Samaki.

Dkt Kantaria ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Elgon Kenya, kampeni ya pembejeo nchini, hata hivyo, amesema ASNET imetoa mapendekezo kwa serikali kuhusu bei ghali ya bidhaa za kilimo na ufugaji.

Alisema, muungano huo unataka ushuru unaotozwa pembejeo, vifaa na mashine za zaraa kupunguzwa na ikiwezekana kufutiliwa mbali ili kuletea wakulima afueni, hatua anayohoji itaafikika kupitia uungwaji mkono na wanasiasa.

Kenya huagiza kutoka nje malighafi kutengeneza fatalaiza na dawa kukabiliana na wadudu na magonjwa shambani.

“Ndio, tunaelewa serikali inapitia changamoto za uhaba wa fedha, japo tunaiomba itilie mkazo sekta ya kilimo kupitia bajeti ya kitaifa. Mgao wa asilimia 10, utaleta afueni na kuiimarisha,” Dkt Kantaria akafafanua.

Sekta ya kilimo inachangia thuluthi moja (1/3), katika ukuaji wa uchumi wa nchi – GDP.

Imegatuliwa kupitia Katiba ya sasa, iliyoidhinishwa 2010, hivyo basi serikali za kaunti zinapaswa kuongoza oparesheni kuiboresha.

Wakulima na wafugaji wanalalamikia kupuuzwa na serikali.

Mfumko wa bei ya bidhaa za kilimo na ufugaji, hata hivyo ni kero ya kimataifa, hasa baada ya janga la corona kulipuka.