Connect with us

General News

Wanasiasa wasifu marehemu Kibaki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanasiasa wasifu marehemu Kibaki – Taifa Leo

Wanasiasa wasifu marehemu Kibaki

CECIL ODONGO Na BENSON MATHEKA

WANASIASA na marafiki wa Hayati Mwai Kibaki jana Jumamosi waliungana kumsifu rais huyo wa tatu wa Kenya wakimtaja kama baba wa Kenya ya kisasa, kwa msingi alioweka wa kukuza uchumi wa nchi.

Katika hotuba yake iliyochukua dakika saba pekee, Rais Uhuru Kenyatta aliwataka wanasiasa waige sifa za uongozi za mtangulizi wake.

“Tuko tayari kuendelea kusaidiana nanyi na Wakenya wote wanawaombea amani mkijua marafiki ni wengi. Hamko pekee yenu kwa kuwa tutaendelea kusimama nanyi,” Rais Kenyatta aliambia familia ya Kibaki.

“Sisi kama Wakenya tusiseme tu kwa vitendo lakini kwa fikira tuige aliyoyatenda huyu mzee. Tunashukuru wananchi wa Othaya na Nyeri kwa jumla kwa kutupa huyu mzee ambaye amehudumia nchi, Afrika Mashariki na dunia nzima. Hatutamsahau,” akasema Rais Kenyatta.

Naibu Rais aligusia siasa kwa kusema ufanisi aliokuwa nao Mzee Kibaki kisiasa na huduma kwa nchi unatoa taswira ya mfumo wa kuinua wananchi wa chini maarufu kama ‘Bottom Up’.

“Mzee wetu Mwai Kibaki kutoka kijiji hiki ambacho hakijulikani sana, alijizatiti na kuwa kiongozi bora na rais wa nchi. Iwapo kuna mfano bora wa ‘Bottom Up’ basi lazima tujifunze kutoka kwa maisha ya Mwai Kibaki,” akasema Dkt Ruto huku akishangiliwa na umati.

Dkt Ruto amekuwa akitumia kauli hiyo katika mikutano yake ya kampeni za uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Muthaura alisema maono ya Kibaki yalisaidia sana kufanya Kenya ilivyo kwa wakati huu.

Alisema kuwa Kibaki alifanya mambo yake bila pupa na kwa umakini mkubwa uliowezesha serikali kufanya maamuzi yaliyofaidi raia kwa jumula.

“Aliweka mbele ujenzi wa miundo misingi kwa kuwa alifahamu ndio ufunguo na msingi wa ukuaji wa uchumi na maendeleo,” alisema Bw Muthaura.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga alisema kwamba alishirikiana na Kibaki kuweka msingi wa kukuza uchumi kupitia miradi mikubwa ambayo baadhi ilitekelezwa baada yake kustaafu.

Rafiki ya Kibaki, Balozi Solomon Karanja alikumbuka siku walizokuwa wakisherehekea kwenye klabu ya Kamulus, Uganda.

Akimkumbuka Rais Kibaki kama mtu mwenye moyo wenye huruma, Balozi Karanja alisimulia jinsi Kibaki alivyowasaidia kufika kwenye kilabu hicho na kuwarejesha chuoni baada ya usiku wa burudani.

“Nikiwa waziri mkuu katika serikali ya muungano, nilishauriana kwa karibu na Rais Kibaki na tukaweza msingi wa miradi mingi ya miundomsingi kupitia Baraza la Taifa la Uchumi ambalo tulibuni,” alisema Bw Odinga.

Naibu Rais William Ruto alimtaja Kibaki kama kiongozi aliyekuwa na upekee wa kufanya maamuzi ya kufaidi raia wa kawaida.

Alisema Kibaki aliweza kupunguza gharama ya mbolea na kuimarisha elimu ya juu na vyuo vya kiufundi nchini.

“Msingi wa miradi mingi ya maendeleo ambayo tulitekeleza katika utawala wa Jubilee uliwekwa na Rais Kibaki,” alisema Dkt Ruto.