Connect with us

General News

Wanasiasa waweke wazi hali zao za afya kabla wawanie – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanasiasa waweke wazi hali zao za afya kabla wawanie – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Wanasiasa waweke wazi hali zao za afya kabla wawanie

Na WANDERI KAMAU

KABLA ya kifo chake mapema mwaka huu 2021, aliyekuwa mbunge wa Juja, Bw Francis Waititu (Wakapee) alisema kuwa viongozi wengi nchini wanaficha Wakenya kuhusu hali zao za afya.

Kwenye mahojiano na gazeti moja baada ya kurejea Kenya kutoka India alikopokea matibabu kutokana na maradhi ya saratani, Bw Waititu alieleza kushtushwa na idadi kubwa ya wabunge aliokutana nao wakipokea matibabu kwa maradhi yayo hayo.

Alisema wengi walimweleza kuwa hawangependa Wakenya kufahamu wanakougua ili kulinda maslahi yao ya kisiasa.

Kauli ya mbunge huyo iliibua uhalisia ambao umekuwepo kwa muda mrefu—wanasiasa wengi huwahadaa raia kuhusu hali zao za afya.

Ni sababu hiyo inachangia wanasiasa nchini kufariki ghafla ama katika hali tatanishi.

Katika nchi zilizostawi kiuchumi, viongozi huwa kama “mali” ya raia na taifa husika.

Raia hupewa taarifa za viongozi wao kwa kina—bila kujali ikiwa viongozi wanataka zitolewe kwa umma au la.

Ni mtindo ambao umekuwepo kwa muda mrefu.

Vivyo hivyo, umewadia wakati wanasiasa nchini pia wafahamu kuwa wanawakosea wananchi wanapowaficha maelezo muhimu kama maradhi wanayougua.

Sababu kuu ni kwamba, kama mataifa ya Magharibi, viongozi ni mali ya nchi.

Wanapaswa kufahamu kuwa, maelezo yao ni muhimu sana, kwa kuwa yanaweza kutumiwa kama urejeleo na serikali iliyopo kubuni sera au mikakati ya kukabiliana na janga husika.

Majuzi, Ikulu ya White House ilitoa taarifa ikisema Rais Joe Biden wa Amerika alikuwa akifanyiwa ukaguzi maalum wa kiafya kutoka kwa madaktari. Hatua kama hiyo hujenga uwazi miongoni mwa raia na serikali yao.

[email protected]

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending