Connect with us

General News

Wanaume wastahili chanjo ya HPV, madaktari wasema – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanaume wastahili chanjo ya HPV, madaktari wasema – Taifa Leo

MUME KIGONGO: Wanaume wastahili chanjo ya HPV, madaktari wasema

Na LEONARD ONYANGO

TANGU 2019, serikali imekuwa ikitoa chanjo ya kuzuia virusi vya Human Papillomavirus (HPV) miongoni mwa wasichana wa umri wa miaka 10 ili kuwakinga dhidi ya kansa ya mlango wa uzazi.

Virusi vya HPV huhusika pakubwa katika kusababisha visa vingi vya kansa ya mlango wa uzazi (cervical cancer).
Serikali inalenga kuchanja wasichana 800,000 humu nchini.

Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa wanawake tisa wanafariki kila siku kutokana na aina hiyo ya kansa.

Inaaminika kuwa chanjo ya HPV ina uwezo wa kupunguza vifo vinavyosababishwa na kansa ya mlango wa uzazi kwa asilimia 70.

Lakini sasa wataalamu wanataka chanjo hiyo ianze kutolewa kwa wanaume, haswa miongoni mwa vijana wa kati ya umri wa miaka 10 na 26.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Texas nchini Amerika, umebaini kuwa virusi vya HPV pia husababisha kansa ya mdomo na umio (oropharyngeal cancer).

Watafiti hao wanasema kuwa asilimia 70 ya visa vya kansa ya umio husababishwa na virusi vya HPV.

Wanapendekeza kuwa vijana wa kiume wa kati ya umri wa miaka 11 na 26 wapewe chanjo ya HPV ili kupunguza visa vya maradhi ya kansa ya umio.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha North Carolina Central (Amerika), Chuo Kikuu cha Nairobi, Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) ma Chuo Kikuu cha Dalian cha nchini China, mnamo 2017, ulibaini kuwa Kenya ni miongoni mwa mataifa yaliyo na visa vingi vya kansa ya umio.

Watafiti hao walisema kuwa maradhi hayo yameshika kasi katika maeneo ya Mlima Kenya, kando ya Ziwa Victoria na baadhi ya maeneo ya Bonde la Ufa.

Profesa Nicholas Abinya wa Kitengo cha Matibabu ya Kansa katika hospitali ya KNH anasema kuwa zaidi ya watu 1,300 hupatikana na kansa ya umio kila mwaka hospitalini hapo.

Idadi kubwa ya waathiriwa, hata hivyo, hufariki kutokana na ukosefu wa matibabu na madaktari wa kutosha.