Connect with us

General News

Wanawake Pwani wahimizwa kugombea nyadhifa za kisiasa, wawe kielelezo cha amani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanawake Pwani wahimizwa kugombea nyadhifa za kisiasa, wawe kielelezo cha amani – Taifa Leo

Wanawake Pwani wahimizwa kugombea nyadhifa za kisiasa, wawe kielelezo cha amani

NA FARHIYA HUSSEIN

WANAWAKE  kutoka eneo la Pwani wamezindua kundi jipya linalolenga kuhamasisha wanawake zaidi kuwania viti vya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Kundi hilo la ‘Pwani Women Caucus Group’ lililozinduliwa siku ya Jumatatu limewataka wanawake kuwania viti tofauti vya kisiasa kama vile vya Ugavana na Seneti na sio tu kiti cha Mwakilishi wa Wanawake.

“Wanawake hawapaswi kugombea nafasi moja tu ya kisiasa. Nafasi ya Mwakilishi wa Wanawake ni kiti cha usaidizi kinachosaidia kuwainua wanasiasa wa kike kuwania viti vingine vya juu. Sote tujikakamue,” akasema Mbunge wa Likoni, Bi Mishi Mboko.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Shirika ya kutetea Haki za Binadamu, Haki Africa, Bi Salma Hemed alisema lengo kuu la kundi hilo ni kuhakikisha kuwa katika kaunti sita za pwani watasimamisha mwanamke mmoja anayewania kiti cha ugavana.

“Tunataka kukomesha dhana kwamba wanawake wanatumika kwa urahisi katika vita vya uchaguzi. Tunataka kuhakikisha sisi, wanawake tunakuwa katika nyadhifa za juu za kisiasa katika ukanda wa Pwani,” alisema Bi Hemed akiongeza kuwa ni wakati wa wanawake kuacha dhana kwamba wanaume pekee ndio wanaweza kuwa viongozi wa kisiasa.

Aliwahimiza wanawake waonyeshe mfano bora katika jamii hasa katika suala muhimu la amani.