[ad_1]
Wanawake wataka wapewe kipaumbele kwenye teuzi za vyama
NA MERCY SIMIYU
VIONGOZI wanawake wanataka miungano ya vyama vya kisiasa iwape kipaumbele kwenye mchujo unaotarajiwa kufanyika Aprili.
Mwenyekiti wa Kundi la Wanawake wanaounga mkono ODM, Betty Syengo, alisema kuwa kundi hilo linalenga kuhakikisha kuwa wanawake wanawakilishwa katika nyadhifa zote zitakazoshindaniwa katika uchaguzi mkuu mnamo Agosti.
“Sisi kama Vuguvugu la Wanawake wa Azimio tuna malengo yetu. Tunataka kuhakikisha tunatoa angalau magavana 20 na maseneta 20. Tutaandaa kikao pia na uongozi wa Azimio ili kuomba angalau teuzi tano za moja kwa moja katika nyadhifa za udiwani kwa wanawake katika kila kaunti,” alisema Bi Syengo.
Gavana wa Kitui Charity Ngilu, aliyeongoza akinamama wengine kwenye uzinduzi wa vuguvugu kwa jina “Jeshi la Baba ni Mama” alisema kinyume na siku za nyuma, wanawake wameamua kusimama na kinara wa ODM Raila Odinga.
“Tumejitolea kumpigia debe Raila kwa sababu tunaamini na tunajua amekuwa akiwapa nafasi akinamama kukua kisiasa,” akasema Bi Ngilu.
Waziri huyo wa zamani ambaye aliwahi kuwania urais mwaka 1997, aliwahimiza wanawake wajitokeze kwa wingi na kuomba kura sawa na wanaume.
Kwenye hafla hiyo walimtaka Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i ahakikishe kuwa akinamama wanalindwa wakati wa kampeni.
Aidha, wanataka pia kuweza kufanya mikutano yao bila kuingizwa baridi na washindani wao wanaume.
Katika miaka ya nyuma, wanawake waliowania nyadhifa za kisiasa walilalama kukejeliwa, kutukanwa au hata kuvurugiwa mikutano na makundi ya vijana wa kukodishwa na wapinzani wanaume.
Baadhi ya wanachama wa vuguvugu wakati wa hafla hiyo ni aliyekuwa waziri wa Maji, Sicily Kariuki na Gavana wa Nairobi Anne Kananu.
Next article
Wanaokosa kulipa mikopo ya Sacco kuingia CRB
[ad_2]
Source link