Connect with us

General News

Wandani wa Kalonzo wapuuzilia mbali ‘njama’ ya mapinduzi ya kisiasa Ukambani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wandani wa Kalonzo wapuuzilia mbali ‘njama’ ya mapinduzi ya kisiasa Ukambani – Taifa Leo

Wandani wa Kalonzo wapuuzilia mbali ‘njama’ ya mapinduzi ya kisiasa Ukambani

Na CHARLES WASONGA

WANDANI wa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka wamepuuzilia mbali uvumi kwamba magavana watatu wa eneo la Ukambani wanapanga kumpokonya taji la kigogo wa siasa za eneo hilo.

Wakiongozwa na Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior, viongozi hao Jumatano walisisitiza kuwa chama hicho hakitishwi na uvumi kama huo ambao hauna msingi wowote.

“Mheshimiwa Stephen Kalonzo Musyoka anasalia kuwa kigogo wa siasa na msemaji wa eneo la Ukambani. Kwa hivyo, tungependa kuwaambia watu wanaotoa madai hayo kwamba wanaota mchana,” seneta huyo akasema kwenye kikao na wanahabari katika makao makuu ya Wiper, Karen, Nairobi.

“Sisi ndio viongozi kutoka eneo hilo na tunawaeleza kuwa Kalonzo hatishiwi na yeyote. Kalonzo hahitaji kuthibitisha kuwa yeye ndiye kigogo wa siasa za Ukambani,” seneta huyo ambaye ni kiranja wa wachache katika seneti, akaongeza.

Magavana watatu, Alfred Mutua (Machakos), Charity Ngilu (Kitui) na Profesa Kivutha Kibwana, Jumatano asubuhi walifanya mkutano mjini Machakos.

Walitarajiwa kutoa taarifa kuhusu siasa za urithi wa urais kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Bw Kilonzo Junior, ambaye alikuwa ameandamana na maseneta, Enock Wambua (Kitui), Agnes Kavindu (Machakos), wabunge na madiwani kutoka kaunti tatu za Ukambani, alitangaza kuwa viongozi wote wa eneo hilo wamealikwa katika mkutano nyumbani kwa Bw Musyoka, Yatta, Jumamosi wiki hii.

Seneta wa Kaunti ya Kitui Enock Wambua akihutubu katika makao makuu ya Wiper mtaani Karen jijini Nairobi, Januari 12, 2022. PICHA | CHARLES WASONGA

Bw Kilonzo Junior ambaye alisoma taarifa kwa niaba ya wenzake alifafanua kuwa ni katika mkutano huo ambapo viongozi watatoa mwelekeo kwa raia kuhusu siasa za 2022.

“Magavana hao watatu na viongozi mbalimbali kutoka eneo la Ukambani wamealikwa katika mkutano wa Jumamosi kule Yatta Farm, kaunti ya Machakos. Wao ni viongozi wa kisiasa, wataalamu, viongozi wa kidini, viongozi wa makundi ya vijana, wazee na akina mama miongoni mwa wengi,” akaeleza.

Naye Seneta Wambua akaongeza: “Mkutano wetu wa Jumamosi utatumiwa kujadili na kutoa mwelekeo kwa jamii yetu kuhusiana na mwelekeo wa siasa ambao tunatarajia kuchukua katika siasa za kitaifa.”

Wakati huo huo, wandani hao wa Bw Musyoka walisema chama cha Wiper kiko imara na hakina wasiwasi wowote kuhusiana na madai kuwa vyama vya ANC na Ford Kenya vinapanga kufanya kazi na mrengo wa Naibu Rais William Ruto.

“Tungependa kuwahakikishia wafuasi wetu kuwa Wiper haijaingiwa na dukuduku kufuatia kuchipuza kwa madai kuwa baadhi ya wanachama wa ANC wanasongea chama cha United Democratic Alliance (UDA). Tuko imara ndani ya muungano wa One Kenya Alliance (OKA) na hatutishiki,” akasema Bw Wambua.