Connect with us

General News

Wandani wa Ruto motoni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wandani wa Ruto motoni – Taifa Leo

Wandani wa Ruto motoni

WALTER MENYA NA LEONARD ONYANGO

WANDANI kadha wa Naibu Rais William Ruto wanakabiliwa na hatari ya kukamatwa na kushtakiwa kwa ufisadi, kulingana na ripoti ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).

Tume hiyo sasa inasubiri idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kabla maafisa wake kuwakamata na kuwafungulia mshtaka Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na Seneta wa Bomet Dkt Christopher Langat.

Mwandani mwingine wa Dkt Ruto Gavana wa Kwale Salim Mvurya hata hivyo atakwepa kukamatwa baada ya EACC mnamo Januari kufunga faili ya uchunguzi dhidi yake kuhusiana na malipo ya Sh13 milioni kwa Baraza la Magavana (CoG). Tume hiyo iliishauri kaunti ya Kwale kufuata kanunu zilizowekwa katika kutoa malipo hayo.

Katika ripoti iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali jana, Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC Twalib Mbarak alisema wanakabiliwa na hatari ya kukamatwa na kushtakiwa kwa ufisadi.

Tume hiyo ilikamilisha uchunguzi dhidi ya Bi Waiguru mnamo Desemba 2021. Uchunguzi huo unahusiana na tuhuma za matumizi mabaya ya mamlaka ya afisi kwa kupokea Sh10.6 milioni kama marupurupu ya ziara feki.

“Wapelelezi wa EACC walichunguza ziara 12 za kimataifa na kugundua kuwa kulikuwa na stakabadhi zilizoonyesha kuwa gavana alialikwa kwa ziara hizo. Lakini hakukuwa na stakabadhi za kuonyesha kuwa maafisa wengi wa kaunti pia walijumuishwa katika ziara hizo. Uchunguzi ulionyesha kuwa maafisa hao waliteuliwa kujumuishwa katika ziara hiyo bila kutumiwa stakabadhi zozote,” EACC ikasema katika ripoti hiyo.

Katika mapendekezo yake kwa DPP, tume hiyo inataka Bi Waiguru na Afisa Mkuu wa Kifedha katika Kaunti ya Kirinyaga washtakiwe kwa kosa la kupanga njama ya kushiriki ufisadi na kutoa taarifa za uwongo kwa maafisa wake.

Ziara hiyo inayodaiwa kuwa feki ni miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na madiwani walipomtimua Bi Waiguru mnamo Juni 2020 kabla ya kurejeshwa afisini na maseneta.

Bi Wauguru alidai kupokea marupurupu ya kuzuru Amerika, Uingereza, Ufaransa, Morocco, India, Ujerumani na Abu Dhabi lakini madiwani walishikilia kuwa hakusafiri.

Maafisa wengine watashtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya afisi, kufeli kuzingatia sheria inayosimamia matumizi ya fedha za umma na uwajibikaji kwa fedha hizo.

EACC ilisema sasa inasubiri majibu kutoka kwa Bw Haji kuhusu faili za uchunguzi ilizowasilisha kwa afisi yake.

Bi Waiguru aligura Jubilee na kujiunga na chama cha United Democratic Alliance (UDA) kwa matumaini ya kuhifadhi kiti chake cha ugavana wa Kirinyaga. Anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Mbunge Mwakilishi wa Kirinyaga Wangui Ngirici na Kiongozi wa Narc- Kenya Martha Karua.

Bw Kuria ambaye amerejea nchini juzi baada ya kupokea matibabu Dubai anakabiliwa na kesi tatu za wizi wa Sh3.7 milioni fedha za Hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge (CDF), Gatundu Kusini.

Naye Seneta Lang’at anakabiliwa na tuhuma za kutoa zabuni kadhaa kwa kampuni moja inayomilikiwa na mkewe. Kwa mfano, kampuni hiyo Isel Creative Design ilipewa zabuni ya thamani ya Sh600,000 ya kuiuzia afisi ya seneta huyo fanicha.

Tume ya EACC inataka Seneta Lang’at afunguliwe mashtaka ya kutoa kandarasi kwa upendeleo, matumizi mabaya ya mamlaka. Tume hiyo pia inapendekeza wakurugenzi wa Isel Creative Design washtakiwe kwa kujipatia mali ya umma kwa ulaghai.

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ilirejesha faili kwa EACC ikitaka uchunguzi dhidi ya seneta huyo ufanywe kwa kina kabla ya kumnyaka.

Hayo yanajiri huku Naibu wa Rais akidai kuwa serikali inatumia taasisi kama vile EACC na Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) kuhangaisha wandani wake huku Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 ukikaribia.

Dkt Ruto ambaye leo anasafiri pamoja na ujumbe wake wa watu 31 kuelekea nchini Uingereza, alipokuwa Amerika alidai kwamba serikali inatumia vitisho na kifua kujaribu kuingiza kinara wa ODM Raila Odinga mamlakani.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending