Connect with us

General News

Wapiga kura watumie busara kuchagua viongozi wastaarabu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wapiga kura watumie busara kuchagua viongozi wastaarabu – Taifa Leo

KINYUA BIN KING’ORI: Wapiga kura watumie busara kuchagua viongozi wastaarabu

NA KINYUA BIN KING’ORI

USTAWI wa nchi yoyote ile hutegemea ukomavu wa viongozi waliochaguliwa kushikilia nyadhifa mbalimbali.

Wanasiasa hutumia kila mbinu kuhakikisha wamechaguliwa,huku baadhi yao wakitoa kauli zinazokosa ustaarabu, heshima na demokrasia katika siasa zetu.

Uhuru na demkorasia ya kisiasa tunaojivunia nchini zinafaa kulindwa kwa kuhakikisha tunazingatia maadili ya umoja, upendo na amani katika taifa letu.

Nimekuwa nikijiuliza kwa nini wananchi wanapenda kushabikia viongozi wenye hulka ya kutoa kauli zinazoweza kuchochea uhasama wa kikabila baina ya Wakenya?

Kwani matamshi ya kishenzi yamekuwa sera katika siasa zetu?

Wananchi wanafaa kuchukua hatua katika uchaguzi mkuu ujao waamue kuwakataa viongozi wachochezi, wakabila, wanafiki na waliofeli kutekeleza ahadi zao kikamilifu.

Uchaguzi ujao uwe wa mabadiliko ambapo wanasiasa wasiojua manufaa ya kuwa viongozi ila kupayuka katika hafla za kisiasa au mazishini watachujwa.

Maadamu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haina mamlaka wa kuwazuia viongozi hao kuwania nyadhifa mbalimbali ni raia tu wanaweza kuwazima viongozi wakorofi katika siasa zetu kwa kuwachagua viongozi wangwana na waadilifu, ili kuleta nidhamu na heshima katika wanasiasa.

Mara nyingi, imekuwa vigumu kuelewa kile wanasiasa wanazungumza katika mikutano yao ya kisiasa,mfano kusema mwanasiasa fulani hafai kuchaguliwa kuwa Rais na jamii fulani kwa sababu hajatahiriwa wala sijui hajaokoka na kadhalika, huo si ukosefu wa sera na adabu?

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending