Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Laikipia Cate Waruguru amesema kuwa naibu Rais William Ruto hafai kuwa rais kwa ajili ya tabia fulani ambazo anazo
Kwenye ujumbe wake kupitia Inooro TV, Waruguru alisema Ruto sio kiongozi wa kusamehea kwa wepesi wanaomkosea, ni mtu mwenye kinyongo moyoni, chuki imemjaa kupindukia.
Waruguru aliongezea kwa kusema kuwa Ruto anafaa kuchukua muda wake, na aige mambo kadhaa kutoka kwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga iwapo anataka kuwa rais.
” William Ruto ni mtu ambaye sio mwepesi wa kusamehea, huonyesha hadharani kuwa mtu mwenye kinyongo moyoni, kwa hivyo mimi naonelea hafai kuwa rais,” Waruguru alisema kwa lugha ya Kikuyu.
Itakumbukwa kuwa Waruguru alikuwa mwandani wa karibu wa Ruto ila mambo yalibadilika hivi majuzi baada ya yeye kufanya mkutano na Raila nyumbani kwake.