Connect with us

General News

Washukiwa 3 wa ugaidi kukaa seli wiki tatu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Washukiwa 3 wa ugaidi kukaa seli wiki tatu – Taifa Leo

Washukiwa 3 wa ugaidi kukaa seli wiki tatu

NA BRIAN OCHARO

WASHUKIWA watatu wa ugaidi waliokamatwa katika Kaunti ya Lamu, wamezuiliwa kwa siku 21 huku polisi wakiendelea kuwachunguza.

Athuman Swaleh, Jackson Konzi na Ali Barow Tirrifo wamedaiwa wana taarifa ambayo inaweza kuwasidia wapelelezi.

Walifikishwa Jumatatu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mombasa Ritah Orora, ambapo ilidaiwa wakiachiliwa kwa dhamana huenda wakavuruga ushahidi.

Hawakupinga ombi la kuwazuilia bali walijitetea kuwa wao ni wakulima na wachuma asali.

Swaleh na Tirrifo walijitetea kuwa wao ni askari wa akiba, na kwamba walikuwa wakiendelea na shughuli zao walipokamatwa.

Polisi wa kikosi cha kupambana na ugaidi (ATPU) pia wamepeleka simu za mkononi za washukiwa hao kwa uchunguzi zaidi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending