Connect with us

General News

Washukiwa watatu wa mauaji ya mwanafunzi wa JKUAT kusalia rumande siku 14 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Washukiwa watatu wa mauaji ya mwanafunzi wa JKUAT kusalia rumande siku 14 – Taifa Leo

Washukiwa watatu wa mauaji ya mwanafunzi wa JKUAT kusalia rumande siku 14

NA LAWRENCE ONGARO

WASHUKIWA watatu wa mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta (JKUAT) Juja, wamekanusha shtaka hilo mbele ya mahakama ya Thika.

Joseph Ndung’u, Kefa Mwaniki, na Paul Mbatha, walifikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Thika, Bw Oscar Wanyaga.

Walipofikishwa mahakamani hawakutakiwa kujitetea bali walisomewa mashtaka ili uchunguzi ufanywe.

Afisa wa upelelezi kutoka kituo cha polisi cha Juja Bw Peter Kaibiru aliiomba mahakama washtakiwa wazuiliwe kwa siku 14 ili uchunguzi uzidi Kufanywa kuhusiana na mauaji hayo.

Wanadaiwa kutekeleza uhalifu huo Aprili 19, 2022. Joel Juma ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne JKUAT, Juja katika kaunti ya Kiambu aliuawa alfajiri hiyo.

Afisa wa upelelezi Bw Kaibiru alitaka mahakama iwazuilie washukiwa kwa muda wa siku 14 ili uchunguzi ufanywe kikamilifu.

Hakimu aliamua kwamba watatu hao watarudishwa mahakamani Mei 5, 2022, wakati mashataka kamili yatawasilishwa hapo kortini.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending