Connect with us

General News

Wasichana waliojifungua warejeshwa shuleni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wasichana waliojifungua warejeshwa shuleni – Taifa Leo

Wasichana waliojifungua warejeshwa shuleni

Na BRIAN OJAMAA

WASICHANA zaidi ya 800 waliojifungua mapema katika Kaunti ya Bungoma wamerejeshwa shuleni baada ya viongozi eneo hilo na timu ya maafisa wa usalama kuingilia kati.

Baadhi ya wasichana waliokuwa katika shule za msingi na za upili walikuwa wameozwa lakini sasa wamerudishwa ili kuendelea na masomo yao.

“Wanajamii waliripoti katika afisi yangu kuhusu wasichana waliotoweka na hapo maafisa wangu wakachukua hatua pamoja na afisi ya kushughulikia maslahi ya watoto, usimamizi wa eneo hili na maafisa wa elimu na wakaweza kuwasaidia kurejea madarasani,” alisema Mwakilishi Mwanamke Catherine Wambilianga.

Alifichua kuwa wasichana zaidi ya 6,000 wamepachikwa mimba tangu kuzuka kwa gonjwa la Covid-19 nchini mnamo Machi 2020.“Kuna wale waliojifungua tayari na kuna waliotungwa mimba baadaye. Tumehusisha wataalam kuwaelekeza na kuwashauri.

Baadhi walirejea shule baada ya kuzaa,” alisema katika eneo la Tongaren.Bi Wambilianga alisema kuwa waendeshaji boda boda ni miongoni mwa idadi kubwa ya wahusika wa tendo hilo haramu.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending