Connect with us

General News

Watu saba wafariki dunia baada ya matatu kukanyaga kilipuzi Mandera – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Watu saba wafariki dunia baada ya matatu kukanyaga kilipuzi Mandera – Taifa Leo

Watu saba wafariki dunia baada ya matatu kukanyaga kilipuzi Mandera

FARHIYA HUSSEIN na MANASE OTSIALO

WATU saba wamethibitishwa kufariki dunia huku 13 wakiwa wanauguza majeraha baada ya matatu iliyokuwa imewabeba kukanyaga kilipuzi Mandera, Jumatatu asubuhi.

Waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mandera.

Matatu hiyo ya nafasi ya abiria 14 hubeba abiria katika maeneo ya Mandera na Arabia. Ilikuwa imetoka Arabia saa kumi na mbili asubuhi ilipokanyaga kilipuzi katika sehemu iliyo kilomita nane kutoka mji wa Mandera.

Manusura mmoja amesimulia hali iliyokuwa.

“Niliabiri matatu katika mji wa Arabia kuelekea Mandera ninakoendesha biashara ya duka. Tulikuwa tunakaribia kuingia kwa barabara ya lami tukio hili la kuogofya lilipotokea,” Bw Abdi Dube amesema.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya Kaunti ya Mandera Abdi Maalim amesema hospitali ya rufaa imepokea miili saba na majeruhi 13 ambapo wanne kati yao wako katika hali mbaya.

Naye mkuu wa polisi eneo la Kaskazini Mashariki Bunei Rono amesema mshukiwa amekamatwa na anapelelezwa.

Kwa mujibu wa polisi, shambulio lilitekelezwa na genge la wahalifu sita.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending