Hospitali ya Pumwani ambapo wauguzi 15 walinasa COVID-19. Picha: Photo: TUKO.co.ke. Source: Original
Onchari alisema wauguzi hao hawakuonesha dalili zozote za kuugua virusi hivyo na kwamba hamna kisa chochote za maafa ya mgonjwa.
“Siwezi sema idadi kamili ya wahudumu wa afya katika hospitali hiyo ambayo wameambukizwa maradhi hayo. Lakini naweza tu kuzungumza kwa niaba ya wauguzi na kuthibitisha 15 kati yao wameambukizwa virusi hivyo,” mwenyekiti huyo alisema kulingana na ripoti ya Nairobi News.
Daktari huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika hospitali ya Nairobi South alipoteza maisha yake Ijumaa, Julai 10 na kuzikwa Jumatatu, Julai 13.
Doreen Lugaliki alikuwa daktari wa kwanza kuangamizwa na coronavirus. Picha: Doreen Lugaliki. Source: Facebook
Aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 38 na alitajwa na wenzake kama daktari mwenye bidii aliyejitolea kazini.
Muungamo wa Matabibu, Wanafamasia na madaktari wa meno (KMPDU) ulitoa wito kwa serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwalinda wahudumu wa afya ambao wanahtarisha maisha yao kufuatia kifo cha Lugaliki.
Mnamo Jumamosi, Julai 11, Wizara ya Afya na KMPDU ilisema daktari mmoja amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kunaswa na virusi hivyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.