Connect with us

General News

Wauzao ‘gesi hewa’ wajipata taabani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wauzao ‘gesi hewa’ wajipata taabani – Taifa Leo

Wauzao ‘gesi hewa’ wajipata taabani

NA RICHARD MUNGUTI

WASHUKIWA wawili wa ulaghai wameshtakiwa kupokea Sh100,000 kwa kudanganya walikuwa na uwezo wa kumuuzia mfanyabiashara mitungi 60 ya gesi.

Justine Murungi na Ruth Muthoni Macharia walikana mbele ya hakimu mkazi Bw Renee Kitangwa kwamba walitumia mtandao wa Facebook kutangaza biashara yao ya kuuza mitungi ya gesi.

Walidai walikuwa wanaendeleza biashara hiyo katika eneo la Makupa, kaunti ya Mombasa.

Katika habari walizosambaza mitandaoni wawili hao walidai walikuwa na uwezo wa kuuza mitungi mingi ya gesi.

Walidaiwa walikuwa na uwezo wa kumuuzia Robert Isiche mitungi 60 ya gesi.

Walimtaka awatumie pesa kwa Mpesa ndipo gari lao limsafirishie mitungi hiyo.

Washtakiwa walidaiwa kutumia nambari ya kitambulisho cha Kevin Brian Bundi Mwangi kuandikisha akaunti ya Mpesa.

Pia walishtakiwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine kutekeleza uhalifu.

Wawili hao walidaiwa kutumia kitambulisho hicho kati ya Deswemba 3 ,2021 hadi Aprili 22, 2022 walipokamatwa.

Murungi na Muthoni walikana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 pesa taslimu kila mmoja.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending