Connect with us

General News

Waziri asema wauguzi hawakufeli mtihani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waziri asema wauguzi hawakufeli mtihani – Taifa Leo

Waziri asema wauguzi hawakufeli mtihani

Na FLORAH KOECH

Waziri wa Leba, Bw Simon Chelugui, amepuuza madai ya mwenzake wa Afya, Bw Mutahi Kagwe kwamba wauguzi 300 kutoka Kenya walifeli mtihani wa lugha ya Kiingereza.

Majuzi, Bw Kagwe alidai kwamba ni wauguzi 10 pekee kati ya 300 waliofanya mtihani huo, ambao ulikuwa hitaji la wauguzi hao kupata kazi Uingereza, waliofaulu.Bw Chelugui, hata hivyo alitofautiana naye akisema kwamba baadhi ya waliotakiwa kufanya mtihani huo hawakuufanya au kupokea majibu yoyote.

Alisema wauguzi hao walipaswa kufanya mtihani wa lazima ambako wanafunzwa na kutahiniwa kuhusu kazi ya uuguzi kimataifa.“Tulisafiri hadi Uingereza na Rais Uhuru Kenyatta Agosti ambako nilitia saini mkataba wa ushirikiano kupeleka zaidi ya wauguzi 20,000 kutoka Kenya,” alisema Bw Chelugui.

“Baada ya kutia saini mkataba huo, tulitangaza kazi na tukapokea maombi 3,500 kutoka kote nchini ambao walitaka kufanya kazi Uingereza. Baadaye, tuliwasilisha orodha kwa wizara ya Afya kuthibitisha iwapo wamehitimu na kupata mafunzo sawasawa na wakarudisha majina ya wauguzi 2,600 na nina furaha tulitoa baadhi ya wataalamu bora,” aliongeza.

Alisema baada ya kuwaachilia, ni lazima wafanye mtihani wa Kiingereza, mtihani wa kompyuta na kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.“Iwapo walifeli au la, bado hatujafika hapo kwa sababu bado hatujawapeleka kufanya mtihani na sifahamu iwapo kuna matokeo yoyote.

Tunaandaa waliofunzu kwa mchakato huo wiki ijayo na baada ya hapo wataweza kusafiri ng’ambo,” alisema waziri Chelugui.Kulingana na Chelugui, awamu zilizobaki ni kuwatuma kufanya mtihani kupitia Baraza la Uingereza, mtihani wa kompyuta unaohusiana na kazi yao, uchunguzi wa matibaby ambao hufanywa na shirika la kimataifa kuhusu uhamiaji na orodha hiyo itawasilishwa kwa wizara ya leba na Ubalozi wa Uingereza ambayo itatayarisha viza vyao waweze kusafiri.

“Nafasi za kazi ni nyingi ng’ambo na wauguzi kutoka Kenya watakuwa wakilipwa Sh300,000 kwa mwezi na watapatiwa nyumba kwa miezi mitatu bila malipo, huduma za matibabu na watoto wao pia watapata shule Uingereza,” alisema.

“Tunatazamia kupata nafasi za kazi katika sekta nyingine. Ninataka kuhimiza wauguzi waliochaguliwa kujiandaa kwa mitihani hii.” ili waweze kupita na kupata nafasi hii inayotamaniwa na watu wengi,” aliongeza Chelugui.