Virusi vya corona vimezidi kuwa tishio kwa Wakenya kila kuchao kutokana na idadi ya watu wanaombukizwa mardhi hayo hatari ambayo yametikisa ulimwengu mzima.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza maambuziki mengine 688 ya COVID-19 katika saa 24 zilizopita na kufikisha idadi ya wagonjwa Kenya kufika 12,750.
Waziri Mutahi Kagwe alithibitisha visa vingine 688. Picha: MoH. Source: UGC
Waziri huyo alitoa takwimu hizo mpya akiwa kaunti ya Embu mnamo Jumamosi, Julai 18.
“Ili kudhibiti msambao wa virusi hivi ni lazima kila mmoja wetu ajukumike kibinafsi. Sasa hivi tunasema…niokoe….nikuokoe. Chukua jukumu la kuwaokoa wazazi wako, marafiki zako na mtu mwingine yeyote,” Kagwe alisema.
Waziri huyo alitangaza kuwa sampuli 4, 522 vilipimwa katika saa 24 zilizopita na kutibitisha wanaume 425 wakiwa wameambukizwa na wanawake 263.
Wakati uo huo alisema wagonjwa wengine watatu wameaga dunia huku 457 wakiripotiwa kupona.
“Watu 457 wamepata nafuu na kufikisha idadi ya waliopona 4,440 kwa jumla. Kati yao 401 walikuwa wakipokea huduma wakiwa nyumbani huku 56 wakiondoka hospitalini,” alidokeza.
Kagwe aliwashutumu wanasiasa kwa kuendelea kuandaa mikutano na kukaidi amri ya Rais Uhuru Kenyatta.
“Ningependa kuwaonya watu dhidi ya kuhudhuria hiyo mkitano ya hao wanasaiasa kwa kuwa ukianza kugonjeka hutawaona. Wanasiasa wameambukiza watu virusi na kukana kabisa. Kwa hivyo, iwapo utasusia mikutano yao watakosa wa kuhutubia na wachoke, wanaitisha mikutanoi kwa sababu wanajua watu ni wapumbavu watahudhuria tu,” alidokeza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.