Connect with us

General News

Waziri Matiang’i awajibikie suala la utovu wa usalama Kerio Valley – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waziri Matiang’i awajibikie suala la utovu wa usalama Kerio Valley – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Waziri Matiang’i awajibikie suala la utovu wa usalama Kerio Valley

WATOTO watatu na mchungaji mmoja waliuawa kwa kupigwa risasi walipovamiwa na majangili katika eneo la Tot, Kaunti ya Elgeyo Marakwet Jumapili, wengine sita wakijeruhiwa.

Kufuatia shambulio hilo imeripotiwa kuwa hofu imetanda katika eneo hilo la Bonde la Kerio wakazi wakihama makwao huku shule kadha zikifungwa.

Viongozi kutoka eneo hilo wakiongozwa na Seneta Kipchumba Murkomen na Mbunge wa Marakwet Mashariki Kangongo Bowen wameitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati ili kurejesha usalama katika eneo hilo ambalo limegeuka “bonde la mauti”.

Lakini viongozi hao wasije wakasahau wana wajibu mkubwa wa kumlazimisha Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i awajibikie utovu wa usalama katika eneo hilo.

Wanayo mamlaka ya kumwagiza Dkt Matiang’i kufika mbele ya kamati za Bunge la Kitaifa na Seneti kuhusu Usalama kutoa ufafanuzi kuhusu kero hilo na kuweka wazi mikakati ya kurejesha usalama eneo hilo.

Bw Murkomen na viongozi wenzake wanayo jukwaa katika kamati hizo kumkumbusha Dkt Matiang’i kwamba mnamo Februari 5, 2022 alikutana nao, pamoja na wakuu wa usalama Rift Valley, katika mkahawa mmoja mjini Nakuru na kuahidi kuwa serikali ingemaliza ujangili eneo hilo.